“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Pasaka
Jumanne, Aprili 20, 2021
Juma la 3 la Pasaka
Mdo 7:51-8:1;
Zab 31:3-4,6-8,17,21 (K. 6);
Yn 6:30-35.
YESU ANATOSHA KABISA
Karibuni ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu
asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana bado linazidi kutukumbusha juu ya maana ya
pasaka, na neema tulizopokea kwa kipindi hiki cha Pasaka. Jana, baada ya Yesu
kuwahimiza wale wafausi wake waliokuwa wanamfuata kwa lengo la kupata mikate ya
kula kwamba watafute chakula kisichoharibika chenye kuwaletea uzima, sasa leo
Yesu anapata fursa ya kuwaeleza viongozi wa Kiyahudi kwamba hata wao wanapaswa
kungangania chakula hicho kisichoharibika na kumwomba Yesu awapatie chakula
hicho. Yesu anawaambia kwamba chakula cha namna hiyo huwa kinaombwa kwani
chatoka kwa Mungu. hata kile chakula walichokula kule jangwani ile mana,
wasifikiri kwamba haikutoka kwa Mungu, Mungu ndiye chanzo cha ile mana. Lakini
hii mana ilikuwa ni chakula kisicho cha kudumu-hivyo, katika injili hii, Yesu
anawaambia kwamba waombe kile chakula kidumucho milele kiwezachokuwapatia uzima
wa milele. Na hiki chakula ni yeye mwenyewe.
Ni kweli ndugu zangu Yesu mwenyewe ni chakula. Hili
tunaliona katika fumbo la Ekaristi-hapa tunapata kumla Yesu kweli katika maumbo
ya mkate na divai. Hii ekaristi ni chakula kiwafaacha wasafiri wote, sisi hapa
duniani tunaoelekea katika nchi ya ahadi yaani mbinguni. Wakati waisraeli
wakielekea katika nchi yao ya ahadi, walipewa mana toka mbinguni. Waliokataa
kuila ile mana walikufa kwa njaa jangwani na kushindwa kufika katika nchi ya
ahadi. Ndivyo na sisi ndugu zangu, sisi tulio safarini kuelekea katika nchi ya
ahadi. Tunapewa Ekaristi tutakapokataa kuila, nakwambia tutashindwa kufika
katika nchi ya ahadi yaani mbinguni. Nakwambia utashambuliwa na njaa,
utashambuliwa na shetani, na utaishia kufa tu njiani. Na hii ni kweli. Wengi
tunaokataa kula Ekaristi tunaishia kukata tamaaa au kufia njiani. Hivyo, ndugu
zangu, tuiheshimu vyema Ekaristi. Tuwaheshimu na mapadre wetu pia.
Katika somo la kwanza tunakutana na kifo cha shemasi
Stefano. Yeye kwa kitendo chake cha kukubali kufa shahidi kwa kumtangaza na
kumtetea Kristo chaonesha kwamba yeye alimkubali Kristo. Alimuona kama chakula
chake, alifurahishwa kulishwa neno lake na sakramenti zake. Nasi tunaoshiriki
katika sakramenti hizi tunapaswa kuonesha ujasiri kama wa huyu Stefano. Si
kwamba tunashiriki katika kumla Kristo na kwenye sakramenti zake halafu mwisho
wa siku tunakuwa tena waoga, mtu akikuambia utoe hiki au ufanye utume Fulani
unaogopa. Tujue kwamba Yesu katika Ufunuo anasema kwamba watu waoga hakika
hawataingia katika ufalme wa Mungu (Uf 21:8). Hivyo tuwe na ujasiri
Copyright ©2013-2020 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki:
see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment