MASOMO
YA MISA, APRILI 17, 2021
JUMA
LA PILI LA PASAKA, JUMAMOSI
SOMO
1
Mdo
6:1-7
Hata
siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na
manung'uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao
walisahauliwa katika huduma ya kila siku. Wale Thenashara wakawaita jamii ya
wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani.
Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye
kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili; na sisi tutadumu
katika kuomba na kulihudumia lile Neno. Neno hili likapendeza machoni pa
mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na
Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa
Antiokia; ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka
mikono yao juu yao. Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana
katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab
33:1-2, 4-5, 18-19
(K)Ee
Bwana, fadhili zako zikae nasi, Kama vile tulivyokungoja Wewe.
Mpigieni
Bwana vigelegele, enyi wenye haki,
Kusifu
kunawapasa wanyofu wa moyo.
Mshukuruni
Bwana kwa kinubi,
Kwa
kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa. (K)
Kwa
kuwa neno la Bwana lina adili,
Na
kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.
Huzipenda
haki na hukumu,
Nchi
imejaa fadhili za Bwana. (K)
Tazama,
jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojeao
fadhili zake.
Yeye
huwaponya nafsi zao na mauti,
Na
kuwahuisha wakati wa njaa. (K)
SHANGILIO
Yn.
10:27
Aleluya,
aleluya,
Kondoo
wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
SHANGILIO
Yn
6:16-21
Hata
ilipokuwa jioni wanafunzi wake wakatelemka baharini wakapanda chomboni,
wakaanza kuivuka bahari kwenda Kapernaumu. Nako kumekwisha kuwa giza, wala Yesu
hajawafikia. Na bahari ikaanza kuchafuka kwa kuvuma upepo mkuu. Basi wakavuta
makasia kadiri ya maili tatu nne, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari na
kukikaribia chombo; wakaogopa. Naye akawaambia, Ni mimi, msiogope. Basi
wakataka kumpokea chomboni; na mara hiyo chombo kikaifikilia nchi waliyokuwa
wakiiendea.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment