“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya Pasaka
Jumamosi,
APRILI 17,
2021,
Juma
la 2 la Pasaka
Mdo
6:1-7
Zab
33:1-2,4-5,18-19,22
Yn
6:16-21
KUTULIZA
DHORUBA ZETU!
Tafakari
yetu ya neno la Bwana katika siku ya leo naomba tuanze kwa kuliangalia somo la
injili. Katika injili hii, tunakutana na wanafunzi wa Yesu wakiwa peke yao
katika bahari katikati ya dhoruba kali. Wanajitahidi kupambana na dhoruba kwa
nguvu zao bila mafanikio. Ni hadi Yesu anapowafikia ndipo na dhoruba hii inapata
kutulia.
Wakiwa
katika dhoruba, wanafunzi walikumbwa na hofu kubwa. Matumaini yao ya kuokoka yalipotea
kabisa. Hofu iliwafanya hata Yesu alipokuja wakashindwa kumtambua. Wakamuona
kuwa kama msumbufu mwingine anayetaka kuwaongezea matatizo zaidi.
Yaliyowatokea
mitume ndugu zangu yanazidi kututokea na sisi hadi siku ya leo ndugu zangu.
Wengi wetu tumetawaliwa tayari na hofu na matatizo mbalimbali. Duniani kuna
matatizo, lakini tusikubali matatizo yatutawale, na kuishinda imani yetu.
Wanafunzi walipokubali matatizo yakawatawala, hakika walishindwa kusaidika, na
hata Yesu anapokuja kwao, wanashindwa kumtambua kama Mwokozi; anawafanya
waongezewe hofu zaidi.
Matatizo
hayapaswi kutawala uhuru wetu. Wapo baadhi yetu ambao kipindi cha matatizo
tunakuwa tayari kufanya kila kitu-tunafanya hata maamuzi ya kijinga. Na wapo
ambao vipindi vya matatizo vimewafilisi kwa sababu ya uzembe wa kuruhusu
matatizo yawatawale. Wapo ambao wameruhusu miili yao kuchanjwa, kufanya hata
matendo ya aibu kwa sababu waliruhusu vipindi vya matatizo vikatawala hata
uhuru wao. Hatupaswi kuwa hivi. Magumu ya maisha yatumiwe kama sehemu ya
kukutana na Bwana.
Katika
somo la kwanza, mitume wanaamua kurudisha utulivu katika jumuiya ya wakristo wa
mwanzo kwa kuwachagua mashemasi watakaohusika na ugawaji wa mahitaji ya kila
siku. Mashemasi hawa walichaguliwa ili kupambana na tatizo la kubaguliwa kwa
baadhi ya wajane katika jamaa. Nyakati zetu pia tunakabiliwa na tatizo la
ubaguzi-ambapo wapo wanaopewa kipaumbele au kupendelewa zaidi. Tunahitaji na
sisi mashemasi watakaosaidia kuondoa ubaguzi wa namna hii. Na sisi tujitolee
kuwa mashemasi wa kupambana na ubaguzi ndani ya jamii zetu. Tuondoe pia kasumba
ya kuwadharau baadhi ya watu na kuwatenga. Wao nao ni binadamu. Yapaswa wapewe
kipaumbele pia. Tumsifu Yesu Kristo.
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment