MASOMO
YA MISA, APRILI 16, 2021
IJUMAA,
JUMA LA 2 LA PASAKA
SOMO
1
Mdo
5:34-42
Lakini
mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamalieli, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa
na watu wote, akasimama katika baraza, akaamuru mitume wawekwe nje kitambo
kidogo, akawaambia, Enyi waume wa Israeli, jihadharini jinsi mtakavyowatenda
watu hawa. Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akijidai ya kuwa
yeye ni mtu mkuu, watu wapata mia nne wakashikamana naye; naye aliuawa na wote
waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu. Baada ya mtu huyo aliondoka Yuda
Mgalilaya, siku zile za kuandikiwa orodha, akawavuta watu kadha wa kadha nyuma
yake, naye pia akapotea na wote waliomsadiki wakatawanyika. Basi sasa
nawaambia, Jiepusheni na watu hawa, waacheni; kwa kuwa shauri hili au kazi hii
ikiwa imetoka kwa binadamu, itavunjwa, lakini ikiwa imetoka kwa Mungu hamwezi
kuivunja; msije mkaonekana kuwa mnapigana na Mungu. Wakakubali maneno yake; nao
walipowaita mitume, wakawapiga, wakawaamuru wasinene kwa jina lake Yesu; kisha
wakawaacha waende zao. Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu
wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo. Na kila siku,
ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari
njema za Yesu kwamba ni Kristo.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Bwana.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab
27:1, 4, 13-14
(K)Neno
moja nimelitaka kwa Bwana, Nikae nyumbani mwa Bwana.
Bwana
ni nuru yangu na wokovu wangu,
Nimwogope
nani?
Bwana
ni ngome ya uzima wangu,
Nimhofu
nani? (K)
Neno
Moja nimelitaka kwa Bwana,
Nalo
ndilo nitakalolitafuta,
Nikae
nyumbani mwa Bwana
Siku
zote za maisha yangu,
Niutazame
uzuri wa Bwana,
Na
kutafakari hekaluni mwake. (K)
Naamini
ya kuwa nitauona wema wa Bwana
Katika
nchi ya walio hai.
Umngoje
Bwana, uwe hodari,
Upige
moyo konde, naam, umngoje Bwana. (K)
SHANGILIO
Kol.
3:1
Aleluya,
aleluya.
Mkiwa
mmefufuliwa na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa
kuume wa Mungu.
Aleluya.
INJILI
Yn
6:1-15
Baada
ya hayo Yesu alikwenda zake ng'ambo ya Bahari ya Galilaya, nayo ndiyo ya
Tiberia. Na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia
wagonjwa. Naye Yesu akakwea mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. Na
Pasaka, sikukuu ya Wayahudi, ilikuwa karibu. Basi Yesu alipoinua macho yake
akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, alimwambia Filipo, Tununue wapi mikate, ili
hawa wapate kula? Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe
atakalotenda. Filipo akamjibu, Mikate ya dinari mia mbili haiwatoshi, kila mmoja
apate kidogo tu. Wanafunzi wake mmojawapo, Andrea, nduguye Simoni Petro,
akamwambia, Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili,
lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa? Yesu akasema, Waketisheni watu.
Na mahali pale palikuwa na majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu
tano jumla yao. Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia
walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. Nao
waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki,
kisipotee cho chote. Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili,
vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia wale waliokula. Basi watu
wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye
ulimwenguni. Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili
wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment