“KUFUFUKA
NA KRISTO”
Tafakari
ya Pasaka
Ijumaa,
Aprili 16, 2021,
Juma
la 2 la Pasaka
Mdo
5:34-42
Zab
27: 1,4,13-14
Yn
6:1-15
KUFAULU
KATIKA JARIBIO LA IMANI!
Mungu
daima anatambua anachopenda kufanya. Daima yeye ana mpango mkamilifu wa maisha
yetu. Leo katika Injili, Yesu anafanya muujiza wa kuwalisha watu kwa mkate na
samaki. Yesu alitambua kwamba ataongeza mkate na samaki ili kuwalisha watu
zaidi ya elfu tano. Lakini kabla ya kufanya hili, anamjaribu Philipo. Hivyo
hivyo Yesu anatujaribu wakati mwingine. Je, hafanyi hivyo?
Majaribio
haya sio kwamba Yesu anapenda kutuuliza tu au kufanya mchezo Fulani na sisi.
Bali, anatupa nafasi ya kudhihirisha imani yetu kwake. Jaribio lililopo kwenye
Injili lilikuwa ni kumfanya Philipo atumie Imani zaidi kuliko kufikiri kwa
kawaida pekee. Philipo aliitwa ili kudhihirisha imani kwamba Mwana wa Mungu
yupo pamoja nao pale. Lakini alishindwa jaribio. Alinyoosha mkono kwa ile hali
ya kutokuwezekana. Lakini katika hali nyingine ni kama Andrea alikuja kuokoa.
Anasema kuna kijana hapa ana mkate na visamaki vichache. Lakini yeye pia alikuwa
na Imani kidogo, aliongeza kusema “lakini vya faa nini kwa umati huu mkubwa
namna hii?”.
Chembe
hii dogo ya imani ya Andrea, ilitosha kwa Yesu kuamuru watu waketi makundi
makundi na hivyo kufanya ule muujiza. Inaonekana kwamba Andrea alikuwa na
ufahamu kidogo kwamba ilikuwa muhimu kutaja visamaki hivi na mkate. Yesu
anavichukua kutoka katika mikono ya Andrea na kuwajali watu.
Mara
nyingi tunajikuta katika hali ngumu na hatujui tufanye nini. Tunapaswa
kujitahidi kuwa na imani kidogo ili Yesu aweze kuwa na kitu cha kutenda katika
maisha yetu. Tunaweza tusiwe na ufahamu wa nini anaenda kufanya, lakini ni
lazima kuwa na ufahamu hata kidogo kwamba Mungu ndiye anaye tuongoza sisi. Kama
tutaweza hata kukuza Imani hii kidogo sisi pia tutashinda majaribio.
Sala:
Bwana, nisaidie niweze kuwa na Imani kamili ya mpango wako ambao unapenda
kuufanya katika maisha yangu. Nisaidie niweze kufahamu kwamba wewe unaongoza na
kuyalinda maisha yangu hata pale ninapo ona maisha yanayumba. Katika hali hizo,
ninaomba Imani ninayo onesha iwe zawadi kwako ili uweze kuitumia kwa utukufu
wako. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment