MASOMO
YA MISA, APRILI 15, 2021
JUMA
LA PILI LA PASAKA, ALHAMISI
SOMO
1
Mdo
5:27-33
Walipowaleta,
wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza, akisema, Je! Hatukuwaamuru
ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza
Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu. Petro
na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. Mungu wa
baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti. Mtu huyo
Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli
toba na msamaha wa dhambi. Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho
Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio. Wao waliposikia wakachomwa mioyo
yao; wakafanya shauri kuwaua.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab
34:1, 8, 15-19
(K)Maskini
huyu aliita, Bwana akasikia.
Nitamhimidi
Bwana kila wakati,
Sifa
zake zi kinywani mwangu daima.
Onjeni
mwone ya kuwa Bwana yu mwema;
Heri
mtu yule anayemtumaini. (K)
Macho
ya Bwana huwaelekea wenye haki,
Na
masikio yake hukielekea kilio chao.
Uso
wa Bwana ni juu ya watenda mabaya,
Aliondoe
kumbukumbu lao duniani.
Walilia,
naye Bwana akasikia,
Akawaponya
na taabu zao zote. (K)
Bwana
yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na
waliopondeka roho huwaokoa.
Mateso
ya mwenye haki ni mengi,
Lakini
Bwana humponya nayo yote. (K)
SHANGILIO
Yn.
20:29
Aleluya,
aleluya,
Umesadiki,
Toma, kwa kuwa umeniona, wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Aleluya.
INJILI
Yn
3:31-36
Yeye
ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya
dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote.
Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali
ushuhuda wake. Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni
kweli. Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu
hamtoi Roho kwa kipimo. Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.
Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali
ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment