“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Alhamisi, Aprili 15, 2021
Juma la 2 la Pasaka
Mdo 5:27-33
Zab 33: 2, 9, 17-20
Yn 3:31-36
KUJAA NEEMAA: NI KUISHI
KATIKA KILE MUNGU ALICHOKUPA!
Ndugu
zangu karibuni kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Tafakari yetu ya
neno la Bwana leo, katika somo la kwanza, Mtume Petro anakiri hadharani kwamba
hawawezi kuacha kumheshimu Mungu na kumheshimu mwanadamu. Viongozi wa Kiyahudi
walikuwa wametoa amri kwamba waache kuhubiri kwa kutumia jina la Yesu. Mitume
wanakataa kufuata amri ya viongozi hawa kwa sababu walikuwa wamepokea amri
kutoka kwa mtawala mkuu zaidi-Yesu Kristo. Amri hii ilikuwa takatifu, hivyo
walishindwa kuacha kuitii.
Kwa
nguvu ya Kristo, waliweza kushukiwa na Roho na pia kufanya miujiza mbalimbli na
kuweza kujipatia furaha kubwa zaidi. Namna hii ilikuwa sio rahisi kwa wao
kuacha kuitii amri ya Mwenyezi Mungu na kufuata ya mwanadamu.
Mitume
hawa wanapaswa kutufundisha jambo muhimu. Wengi wetu tunawatii wanadamu kuliko
Mungu. Tupo tunaowaogopa wanadamu, tunahofia kufukuzwa kazi au kuachwa bila
kuolewa na baadhi wamekuwa tayari hata kubadili dini kwa sababu ya hofu katika
maisha yake. Tunaogopeshwa na wanadamu wenzetu. Yafaa tujifunze kuona ukuu wa
Mungu wetu ndani ya maisha yetu.
Kila
mmoja leo anapaswa kuchunguza kile kinachomtia hofu, kinachomfanya asilale-je,
kinatoka wapi? Ni cha Mungu? Vitu vya namna hii hutufanya tushindwe kumtii
Mwenyezi Mungu. Tunatumia muda mwingi kuviwaza. Havipaswi kutusumbua kiasi
hiki. Lazima tujue kwamba Mungu ana uwezo kuliko mambo haya. Mungu anapaswa
kutawala akili zetu.
Kwenye
somo la injili, Yohane anatuhimiza kumwamini Yesu. Anatueleza kwamba Baba
amempatia mamlaka makubwa juu yake. Hivyo anapaswa kuabudiwa. Asiyemwamini
hakika atapotea. Mitume katika somo la kwanza wametuonesha mfano wa kumwamini.
Yesu
alikabiliwa na upinzani, wapo waliopinga asiabudiwe. Mitume wanaonesha kwa msisitizo
kwamba anapaswa kuabudiwa. Sisi tuzidi kujikabidhi mikononi mwa Yesu wetu. Kila
mmoja aongeze bidii yake ya kumwamini Yesu popote pale alipo. Tuwe watu wa
kuongeza bidii tupate kumwabudu Yesu kwa utakatifu zaidi.
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment