MASOMO
YA MISA, APRILI 14, 2021
JUMA
LA PILI LA PASAKA, JUMATANO
SOMO
1
Mdo
5:17-26
Akaondoka
Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya
Masadukayo), wamejaa wivu, wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza;
lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,
Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu. Nao waliposikia
wakaenda alfajiri hekaluni, wakaanza kufundisha. Akaja Kuhani Mkuu nao
waliokuwa pamoja naye, wakawakutanisha watu wa baraza, na wazee wote wa wana wa
Israeli, wakatuma watu gerezani ili wawalete. Hata watumishi walipofika
hawakuwaona gerezani, wakarudi wakatoa habari, wakisema, Gereza tumeikuta
imefungwa salama, nao walinzi wamesimama mbele ya mlango; lakini tulipoufungua
hatukukuta mtu ndani. Basi jemadari wa hekalu na wakuu wa makuhani waliposikia
haya, wakaingiwa na shaka kwa ajili yao, litakuwaje jambo hilo. Mtu mmoja akaja
akawapasha habari ya kwamba, Watu wale mliowaweka gerezani wako ndani ya
hekalu, wamesimama wakiwafundisha watu. Ndipo yule jemadari akaenda pamoja na
watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawapiga
kwa mawe.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab
34:1-8
(K)
Maskini huyu aliita, Bwana akasikia.
Nitamhimidi
Bwana kila wakati,
Sifa
zake zi kinywani mwangu daima.
Katika
Bwana nafsi yangu itajisifu,
Wanyenyekevu
wasikie wakafurahi. (K)
Mtukuzeni
Bwana pamoja nami,
Na
tuliadhimishe jina lake pamoja.
Nalimtafuta
Bwana akanijibu,
Akaniponya
na hofu zangu zote. (K)
Wakamwelekea
macho wakatiwa nuru,
Wala
nyuso zao hazitaona haya.
Maskini
huyu aliita, Bwana akasikia,
Akamwokoa
na taabu zake zote. (K)
Malaika
wa Bwana hufanya kituo,
Akiwazungukia
wamchao na kuwaokoa.
Onjeni
mwone ya kuwa Bwana yu mwema;
Heri
mtu yule anayemtumaini. (K)
SHANGILIO
Rum.
6:9
Aleluya,
aleluya,
Kristo
akiisha kufufuka, katika wafu hafi tena. Mauti haimtawali tena.
Aleluya.
INJILI
Yn
3:16-21
Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma
Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu
hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru
imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao
yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye
nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye
nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment