"ASALI
ITOKAYO MWAMBANI"
Jumatano,
Aprili 14,, 2021.
Juma
la 3 Pasaka
Kumbukumbu
ya Mt. Yosefu Mfanyakazi
Mdo
5:15-17;
Zab
34:1-8;
Yn
3:16-21.
Baba
alionesha upendo mkubwa sana kwa dunia.
Ndugu zangu karibuni kwa
adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Katika somo la kwanza, wanafunzi wa
Bwana wanaonja wokovu wa Bwana katika maisha yao. Bwana anamtuma malaika wake
kuja kuwaokoa.
Palitokea viongozi wa
Kiyahudi waliowaonea wivu na kuwafunga gerezani. Viongozi hawa waliamini sana
nguvu zao wakitegemea kwamba kila watakachofanya kitafanikiwa kutokana na wingi
wa mamlaka. Lakini leo Mwenyezi Mungu amewaonesha kwamba hakika ni mwenye nguvu
kuliko wao. Hivyo, waache kuwatishia na kuwaonea watumishi wake. Jambo hili
liliwaletea fedheha kubwa viongozi hawa. Nguvu zao zilishindwa kuwapatia sifa
au kuizima kazi ya Bwana. Mungu ni nguvu ya wanyonge.
Somo hili litupatie funzo
la kuacha kujiamini kupita kiasi. Twaweza kuwa na maarifa, akili, pesa,
marafiki, nguvu na hata silaha. Lakini tusipomtegemea Mungu, upo wakati yote
haya yataonekana kuwa bure. Zaidi sana ni kujifunza kugundua ukomo wa uwezo na
mamlaka yetu na hata wa marafiki zetu. wengi wetu hatujui ukomo wao. Hizi ndizo
sababu za wengi wetu kujivuna kupita kiasi.
Injili inatuagiza na
kutuambia kwamba Yesu wetu alikuja ulimwenguni ili kila amwaminiye asipotee
bali awe na uzima wa milele. Baba alionesha upendo mkubwa sana kwa dunia. Sisi
tutambue kwamba bado hatujajitahidi kuonesha upendo mkubwa sana kwa dunia. Bado
vipo vingi ambavyo tungalipaswa kufanya ili kuisadia dunia lakini hatujafanya
bado.
Muda wetu tumeutumia
vibaya, wapo wagonjwa wengi na wengi wenye shida na matatizo ambao wangalipaswa
ukute wamekwishasaidika kwa sababu ya mimi kutumia muda wangu zaidi na kupaaza
sauti yangu zaidi. Labda tuangalie kukaa kwangu kimya kumewafanya watu wangapi
wasaidike?
Hapa kwa hakika
hatujajitoa bado kama inavyotakiwa. Au kama kila mmoja wetu angalikuwa
anachangia kila kwaresma kwa ajili ya kanisa-je, ni watu wangapi tungalikuwa
tumewasaidia. Uvivu wetu umeirudisha dunia nyuma na ndio sababu za wengi wetu
kuwa maskini. Tuongeze majitoleo yetu ili wengine wasaidike. Tuache kukaa
vijiweni. Tunapoteza muda mwingi sana. Ule muda wa vijiweni ungaliweza
kutusaidia kufanya mengi. Wengi wetu tunaishi katika mazingira machafu,
tunaumwa kila siku kwa sababu ya kukosekana kwa wenye kujitolea kuyasafisha.
Tuzidishe majitoleo yetu ili dunia yetu iwe sehemu pema zaidi. Tumsifu Yesu
Kristo
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment