ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Pasaka
Alhamisi, Aprili 22, 2021.
Juma la 3 la Mwaka
Mdo 8:26-40;
Zab 66:8-9,16-17,20 (K. 1);
Yn 6:44-51.
KUVUTWA KWA YESU!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubhui ya leo. Leo bado tunazidi
kujikumbushia juu ya habari zilizoletwa na Kristo mfufuka. Na katika somo letu
la injili, Yesu anazidi kusema kwamba yeye ni chakula cha uzima, na yeyote
atakayekuja kwake hakika hatamuacha bali atamfufua siku ya mwisho. Yesu
anawaeleza kwamba yeye chakula atoacho ni tofauti na ile mana, ile mana
walipoila kule jangwani waliila lakini pia wengi walikufa-ilishidwa kuwafikisha
katika nchi ya ahadi. Hii ni kwa sababu ile mana haikuwa na nguvu, au neema
iwezayo kumfanya mtu asonge mbele. Lakini chakula atoacho Yesu kinatoa neema,
kinakupatia nguvu wewe mwenyewe usonge mbele. Chenyewe ni chanzo cha neema.
Hii
ndio Ekaristi Takatifu ndugu zangu, yenyewe inatoa neema, inakuunganisha na
Mungu, na yeyote apokeaye Ekaristi, kwa moyo kabisa, na kwa imani, nakwambia
mtu huyo si mchezo kamwangalie hata maisha yake, ni tofauti. Ekaristi ina nguvu
ajabu lakini labda sisi hatujaitumia sawasawa kwa sababu tunafanyaga mambo kwa
harakaharaka hasa kwa baadhi ya nyakati katika misa zetu. Lakini wale wakaa
pweke au waherimita wa jangwani waliweza kuishi kwa kula tu ekaristi, waliweza
kubakia na afya tele wakati wowote. Hivyo, sisi tuiheshimu Ekaristi vyema.
Tuipokee, itufanye tubadilike na kuanza upya maishani hasa kwa neema itolewayo
na hii Ekaristi.
Katika
somo la kwanza, tumesikia habari za Philipo akimbatiza Towashi wa Ethiopia.
Huyu alionesha nia na chembe ya Imani kwa kuanza kuyasoma maandiko matakatifu
bila hata ya kuyaelewa. Lakini mara moja Mungu akabariki nia yake kwa kumletea
mfafanuzi aliyemuelezea maana ya anachosoma na mwishowe Imani yake ikakua hata
kubatizwa.
Kama
Yesu alivyosema kwenye injili hakuna aendaye kwake isipokuwa ni Mungu mwenyewe
kamgusa na hili linatokea kwa Towashi huyu. Nasi tunaalikwa leo ndugu zangu,
tuoneshe nia, tena kidogo tu, nakwambia Mungu atabariki mara moja, ukianza tu,
Mungu naye anajalizia. Labda kama mimi ni mlevi na ninataka kuacha, hebu leo
niseme basi sinywi -nakwambia utaona na Mungu mwenyewe atakuongezea nguvu ya
wewe kuacha, au kama mimi siungami-nina miaka kumi na zaidi.
Hebu
leo niweke nia niseme nataka kuungama-utashangaa Mungu ataongezea ya kwake na
utafanikiwa kuungama.
Hivyo,
ndugu zangu kwenye mambo mengi sisi tuweke nia tu nakwambia mambo utashangaa
yakienda tu. Tumsifu Yesu Kristo.
Copyright ©2013-2020 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki:
see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment