MASOMO YA MISA, MACHI 8,
2021
JUMATATU, JUMA LA 3 LA
KWARESIMA
SOMO 1
2 Fal. 5:1-15
Naamani, jemadari wa
jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye
kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake Bwana alikuwa amewapa Washami kushinda;
tena likuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma. Na Washami
walikuwa wametoka vikosi vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka
nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani. Akamwambia bibi yake, Laiti
bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya
ukoma wake. Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana
mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi. Mfalme wa Sahmu akasema,
Haya! Basi, mimi nitampelekea mfalame wa Israeli waraka. Basi akaenda zake,
akachukua mikononi mwake talanta kumi za fedha, na vipande vya dhahabu elfu
sita, na mavazi kumi.
Akampelekea mfalme wa
Israeli waraka ule, kusema, Waraka huu utakapokuwasilia, tazama, nimemtuma
mtumishi wangu Naamni kwako, ili upate kumponya ukoma wake. Ikawa, mfalme wa
Israeli alipousoma waraka, alirarua mavazi yake, akasema, Je! Mimi ni Mungu,
niue na kuhuisha, hata mtu huyu akanipelekea mtu nimponye ukoma wake? Fahamuni,
basi, nakusihini, mwone ya kuwa mtu huyu anataka kugombana nami.
Ikawa, Elisha, yule mtu
wa Mungu, aliposikia kwamba mfalme wa Israeli ameyararua mavazi yake, ndipo
akatuma mtu kwa mfalme, akisema, Mbona umeyararua mavazi yako? Na aje sana
kwangu mimi, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli.
Basi Naamani akaja na
farasi wake na magari yake, akasimama mlangoni pa nyumba ya Elisha. Naye Elisha
akampelekea mjumbe, akisema. Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama
ya mwili wako itakurudia nawe utakuwa safi. Lakini Naaman akakasirika,
akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama,
na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye
ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski,
si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! Siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa
safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira.
Watumishi wake
wakamkaribia, wakamwambia, wakisema, Baba yangu, kama yule nabii angalikuambia
kutenda jambo kubwa, usingalilitenda? Je! Si zaidi basi, akikuambia, Jioshe,
uwe safi? Ndipo akashuka, akajichovya mara saba katika Yordani sawasawa na neno
lake yule mtu wa Mungu; naye nyama ya wmili wak eikarudi ikawa kama nyam aya mwili
wa mtoto mchanga, akawa safi.
Akamrudia yule mtu wa
Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa
tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli, basi
nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako.
Neno la Bwana… Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 42:1-2, 43:3-4 (K)
42:3
(K) Nafsi yangu inamwonea
kiu Mungu, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu.
Kama ayala aioneavyo
shauku mito ya maji.
Vivyo hivyo nafsi yangu
inakuonea shauku, Ee Mungu. (K)
Nafsi yangu inamwonea kiu
Mungu, Mungu aliye hai,
Lini nitakapokuja
nionekane mbele za Mungu? (K)
Niletewe nuru yako na
kweli yako ziniongoze,
Zinifikishe kwenye mlima
wako mtakatifu
Na hata maskani yako. (K)
Hivyo nitakwenda madhabahuni
kwa Mungu,
Kwa Mungu aliye furaha
yangu na shangwe yangu. (K)
SHANGILIO
Yn. 8:12
Mimi ndimi nuru ya
ulimwengu, asema Bwana, Yeye anifuataye, atakuwa na nuru ya uzima.
INJILI
Lk. 4:24-30
Yesu alifika Nazareti
akawaambia makutano hekaluni: Amin, nawaambia ya kuwa, Hakuna nabii mwenye
kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe. Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na
wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa
miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; wala Eliya hakutumwa
kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. Tena,
palikuwa na weny eukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala
hapana aliyetakazwa ila Naamani, mtu wa Shamu.
Wakajaa ghadhabu wote
waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo. Wakaondoka wakamtoa nje ya mji,
wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate
kumtupa chini; lakini yeye alipiita katikati yao, akaenda zake.
Neno la Bwana… Sifa kwako
Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment