MASOMO
YA MISA, MACHI 6, 2021
JUMAMOSI,
JUMA LA 2 LA KWARESIMA
SOMO
1
Mik.
7:14-15, 18-20
Walishe
watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao, mwituni
katikati ya Karmeli; na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale.
Kama katika siku zile za kutoka kwako katika nchi ya Misri nitamwonyesha mambo
ya ajabu.
Ni
nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu
wa urithi wake waliosalia? Hashiki hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia
rehema. Atarejea na kutuhurumia; atayakanyaga maovu yetu; nawe utazitupa dhambi
zao zote katika vilindi yva bahari. Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na
Ibrahimu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
103:1-4, 9-12 (K) 8
(K)
Bwana amejaa huruma na neema.
Ee
nafsi yangu umhimidi Bwana.
Naam,
vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi
jina lake takatifu.
Ee
nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Wala
usizisahau fadhili zake zote. (K)
Akusamehe
maovu yako yote,
Akuponya
magonjwa yako yote,
Aukomboa
uhai wako na kaburi,
Akutia
taji ya fadhili na rehema. (K)
Yeye
hatateta sikuzote,
Wala
hatashika hasira yake milele.
Hakututenda
sawa na hatia zetu,
Wala
hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu. (K)
Maana
mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,
Kadiri
ileile rehema zake ni kuu kwa wamchao.
Kama
mashariki ilivyo mbali na magharibi,
Ndivyo
alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. (K)
SHANGILIO
Yn.
6:64, 69
Maneno
yako, Ee Bwana, ni roho, tena ni uzima; Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
INJILI
Lk.
15:1-3, 11-32
Watoza
ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia Yesu wamsikilize. Mafarisayo
na waandishi wakanung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi,
tena hula nao. Akawaambia mfano huu, akisema, Mtu mmoja alikuwa na wana wawili;
yule mdogo akamwambia babaye, Baba, nipe sehemu ya mali inayoniangukia.
Akawagawia vitu vyake. Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya
vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya
uasherati.
Alipokuwa
amekwisha tumia vyote, njaa kuu iliingia nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji.
Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani
kwake kulisha nguruwe. Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula
nguruwe, wala hapana mtu aliyempa kitu. Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni
watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa
ninakufa kwa njaa. Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba,
nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye
kama mmoja wa watumishi wako. Akaondoka, akaenda kwa babaye.
Alipokuwa
angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia
shingoni, akambusu sana. Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na
mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. Lakini baba aliwaambia watumwa
wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na
viatu miguuni; mleteeni ndama yule aliyenona mkamchinje nje; nasi tule na
kufurahi; kw akuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa
amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.
Basi,
yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba na lipokuwa akija na kuikaribia nyumba,
alisikia sauti ya nyimbo na machezo. Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo
haya, maana yake nini? Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja
ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima. Akakasirika, akakataa
kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. Akamjibu baba yake, akasema.
Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati
wowote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;
lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba,
umemchinjia yeye ndama aliyenona.
Akamwambia,
Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. Tena,
kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuw ahuyu ndugu yako alikuwa amekufa,
naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment