“ASALI
ITOKAYO MWMABANI”
Tafakari
ya Kwaresima
Jumamosi,
Machi 6, 2021,
Juma
la 2 la Kwaresima
Mika
7:14-15,18-20;
Zab
103;1-4, 9-12;
Lk
15: 1-3, 11-32
KUMRUDIA
MUNGU!
Karibuni ndugu zangu kwa
adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana katika asubuhi ya
leo tutaanza kwa kuliangalia somo la Injili ambapo tunakutana na simulizi la
mwana mpotevu. Huyu alingangania sehemu yake ya urithi kwa nguvu, akachukua
mali zake na kwenda kula na makahaba, alimwonesha baba yake tabia mbaya na
dharau na kumlazimisha ampe urithi. Halafu mwishowe mambo yanakuwa magumu na
kuanza kurudi na Baba anampokea.
Simulizi hili
nalifananisha na hali ya sasa iwakumbayo hasa vijana wengi-unakuta kijana awe
wa kike au wa kiume inafika muda fulani, hasikilizi maongozi ya baba yake,
anajidai kuwa na akili kupita kiasi, anatukana hata wazazi wake, hataki hata
kusikia mwongozo wao. Lakini mambo yanakuwa magumu unashangaa anarudi tena kwa
wazazi wake, upole umemjaa kabisa, majivuno yote kwisha na ndio anamtegemea
mama yake ampatie kitu. Hili ni jambo linalotokea-na mzazi anakupokea baada ya
kumwonyesha hivyo majivuno yako. Tumshukuru Mungu kwa upendo tunaooneshwa na
wazazi wetu hawa.
Hapa tujifunze kitu ndugu
zangu: kwanza vijana tuache kujiona kana kwamba sisi ni wajanja kuliko wazazi
wetu, tuache kufikiri kwamba tunayajua maisha kuliko wazazi wetu, au kufikiri
kwamba tunajua kuyafurahia maisha kuliko wazazi wetu-wao wameishi miaka mingi
na wameona mengi. Tusifikiri kwamba ati wamepitwa na wakati-wakikuambia kitu
waweza kuona kama cha kijinga lakini fikiria mara mbili. Kila siku wazazi wetu
wanatusamehe kama Baba wa mwana mpotevu.
Yesu anatumia mfano huu
kufundisha kwamba upendo wa Mungu alionao kwetu ni zaidi hata ya upendo wa
mzazi kwa mtoto-yeye atupenda Zaidi. Somo hili limewekwa kipindi hiki cha
kwaresima ili litufikirishe namna jinsi kila mmoja wetu alivyowahi kuwa mwana
mpotevu mbele ya Mungu, namna kila mmoja wetu alivyoweza kutumia mali, uwezo
wake, viungo vyake alivyopewa na Mungu kwa kumkufuru Mungu. Mfano, ni pale
viungo vyetu vya uzazi vinavyopevuka-na mara moja tunasema sasa vitumike kwa
uzinzi, tunasema sasa ni wakati wa kuvifurahia-hapa ni kuwa kama mwana
mpotevu-hii ni kwa sababu tuliviona vikiwa vidogo, havina kitu, sasa vimechanua
tunajivuna, tunaruka navyo na wakati utafika ambapo vitaishiwa nguvu kabisa na
kuvirudisha kwa baba tukiomba msamaha. Somo hili litufanye sisi vijana tuache
kutapanya urithi wa viungo tulivyonavyo kwa ajili ya uzinzi.
Somo la kwanza nabii Mika atueleza zaidi juu ya upendo
na huruma ya Mungu kwetu sisi. Nasi tuzidi kumrudia Bwana katika kwaresma hii
na kumwomba msamaha hasa kwa kuvitumia viungo vyetu vibaya. Tumsifu Yesu Kristo
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment