“KWARESIMA
YA UKARIMU”
Tafakari
ya Kwaresima
Alhamisi,
Februari,25, 2021.
Juma
la 1 la Kwaresima
Est
C:12, 14-16, 23-25;
Zab
138:1-3, 7-8
Mt:
7:7-12
OMBENI
NANYI MTAPEWA!
Ndugu
zangu wapendwa karibuni kwa adhimisho la Misa Takatifu Asubuhi ya leo. Tukianza
na wimbo wetu wa katikati unaosema siku ile niliokuita uliniitikia ukanitia
nguvu na kunifariji nafsi. Mzuburi anamshukuru Mungu kwani alipokuwa katika
taabu alimwita Bwana naye akawa ndio chanzo cha nguvu na faraja zake.
Wimbo
huu unatilia mkazo somo la kwanza kwani wakati Waisraeli walivyokuwa katika
hatari ya kuangamizwa na Hamani, malkia Esta alifunga na kusali na kweli Mungu
akawafariji waisraeli nafsi kwa kuwaokoa na mkono wa Hamani na akawapa nguvu.
Tukimuomba Bwana vizuri tunapokuwa katika matatizo daima anatusaidia. Hata kama
tunapitia katika magumu ya namna gani yeye atatusikia kama tutamuita vizuri na
kwa moyo.
Somo
la Injili linatilia mkazo tena kwamba wakutusaidia kutua mizigo yetu
tunapoelemewa ni Yesu. Sisi tumuite kwa Unyoofu kama Malkia Esta alivyomuita
Mungu kwa unyoofu. Hakika Mungu hatatuacha. Yeye daima tukimuita vizuri
atatusikia. Mara nyingi pengine Mungu hatusikii kwasababu tunaomba ili Mungu
awalipe visasi wale waliotukosea. Tunatamani kama Mungu angewaangamiza na
kuwaulia mbali. Hatuombi Mungu awabadilishe na kuwafanya wema, ila sisi
tunaomba atue mizigo yetu kwa kuwateketeza maadui wetu na kuwafutilia mbali
kabisa.
Tumuombe
Mungu atusaidie tukimbilie kwake kutuoa mizigo yetu. Tusikimbilie kwa viumbe
wake aliowaumba. Yeye ananguvu na mizigo yetu ataitua hakika. Sisi
tunamkimbilia mganga, tukidhani yeye ndio atatutia nguvu na kutifariji. Ukweli
ni kwamba Bwana ndiye mfariji wetu tumkimbilie yeye Kama Esta alivyofanya
akabarikiwa na Waisraeli wote.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment