MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 25, 2021
ALHAMISI,
JUMA LA 1 LA KWARESIMA
SOMO
1
Est.
4:17
Malkia
Esta naye alimkimbilia Bwana, akishikwa na uchungu wa mauti. Akazivua nguo zake
za fahari akavaa nguo za huzuni, na kilio, na badala ya manukato mazuri
alijitia majivu na samadi kichwani; akajinyenyekesha mwili wake, hata mahali pa
mapambo ya furaha alijifunika kwa nywele zake zilizofumuliwa. Akamwomba Bwana
wa Israeli, akisema:
Bwana
wangu, Wewe peke yako u Mfalme wetu. Unisaidie mimi niliye mkiwa, wala sina
msaidizi wmingine ila Wewe; maana hatari yangu imo mkononi mwangu.
Tangu
nilipozaliwa katika kabila ya jamaa yangu, nimesikia ya kuwa Wewe, Bwana,
ulimchagua Israeli katika mataifa yote, na baba zetu katika jamaa zao, kuwa
urithi wa daima, ukawatimilizia yote uliyoyaahidi.
Utukumbuke,
Ee Bwana; ujifunue wakati wa taabu yetu; unipe moyo thabiti, Ee Mfalme wa
miungu na Bwana wa milki zote. Unitie kinywani mwangu maneno ya kufaa mbele ya
samba, ukaugeuza moyo wake apate kumchukia yule anayepigana nasi, ili akomeshwe
pamoja na wote wenye nia moja naye. Lakini utuokoe sisi kwa mkono wako;
unisaidie mimi niliye peke yangu, bila msaidizi mwingine ila Wewe, Bwana.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
138:1-3, 8-9 (K) 1
(K)
Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
Nitakushukuru
kwa moyo wangu wote,
Mbele
ya miungu nitakuimbia zaburi.
Nitasujudu
nikilikabili hekalu lako takatifu,
Nitalishukuru
jina lako. (K)
Kwa
ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa
amana umeikuza ahadi yako,
Kuliko
jina lako lote.
Siku
ile niliyokuita uliniitikia,
Ukanifariji
nafsi kwa kunitia nguvu. (K)
Na
mkono wako wa kuume utaniokoa.
Bwana
atanitimilizia mambo yangu;
Ee
Bwana, fadhili zako ni za milele;
Usiziache
kazi za mikono yako. (K)
SHANGILIO
Eze.
33:11
Sikufurahii
kufa kwake mtu mwovu, asema Bwana, Bali aiache njia yake mbaya, akaishi.
INJILI
Mt.
7:7-12
Siku
ile Yesu aliwaambia wafuasi wake: Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi
mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye
atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye,
mwanawe akiomwomba mkate, atampa jiwe? Atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa
nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema,
je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Basi
yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hivyo
ndiyo torati na manabii.
Neno
la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment