“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatano,
Februari 10, 2021
Juma
la 5 la Mwaka
Mwa
2: 4-9, 15-17;
Zab
103: 1-2, 27-30;
Mk
7: 14-23.
NDANI
NA NJE!
Ndugu
zangu karibuni kwa tafakari ya neno la Bwana asubuhi ya leo katika adhimisho la
Misa Takatifu. Tafakari yetu inaanza kwa kuiagalia zaburi yetu ya wimbo wa
katikati. Hapa tunamkuta mzaburi akifurahia uumbaji na kuusifu. Anatangaza
kwamba viumbe vyote vimeumbwa na Bwana na vyote ni lazima vimwangalie Bwana ili
apate kuvilisha. Mungu asipofungua mikono yake hakika hivi haviponi. Mwanadamu
ameumbwa ili amwangalie Bwana.
Ndio
ujumbe tunaoukuta tena katika somo la kwanza ambapo tunasikia habari juu ya
uumbaji wa mwanadamu. Yeye anapoumbwa, anapatiwa maagizo maalum, kwamba ale
matunda ya miti yote lakini mti maalumu alioambiwa na Mungu asile matunda yake.
Hili lilikuwa agizo la kiutii, kwamba Mwanadamu alipaswa kumuangalia Mungu
apate kumlisha. Hivyo alipaswa kula kile alichoagizwa na Mwenyezi Mungu.
Sisi
ndugu zangu tutambue kwamba tunalishwa na Mwenyezi Mungu. Hivyo ni lazima
tumtazame yeye kila siku ili apate kutulisha. Wengi wetu hatujui kumtazama
Bwana na ndio maana tunaishi katika njaa. Mwanadamu analishwa na Bwana. Na
wakati tunalishwa na Bwana, lazima tufuate masharti-yeye aliwaambia wazazi wetu
wa mwanzo wasile matunda ya mti wa katikati. Sisi tunaugua kwa sababu ya kula
vilivyokatazwa. Wengi wetu tunateseka sasa, tunakazana kutoa sumu mwilini,
wengine wamepoteza uhai kwa sababu ya kutokufuata masharti. Tuwe watu wa
kufuata masharti na tuwe na utii.
Katika
injili yetu, Yesu anaendelea kuwapinga wafarisayo na waandishi juu ya sheria
zao za kutawadha na za vyakula. Anasema kwamba kile kinachomuingia mwanadamu
hakiwezi kumfanya najisi, ni kile kimtokacho.
Wafarisayo
walipotoka kwa sababu walijali sana kile kilichoingia kuliko kilichotoka moyoni
mwao. Labda waliona afadhali kumdhulumu jirani kuliko kula na mikono
isiyotawadhwa, au walikuwa tayari kumtelekeza mgonjwa kuliko kumgusa na
kujisababishia unajisi. Tabia za namna hii ziliwakosesha mbingu. Sisi tusiwe
kama wafarisayo. Wapo baadhi yetu tulio tayari kutoa michango mikubwa kanisani
lakini nyumbani mwetu wapo mayatima au majirani maskini na hatuko tayari
kuwasaidia. Tuwe watu wa kiroho, wenye kuongozwa na huruma. Tuache kutenda
matendo ya nje ili tuwafurahishe wengine. Sisi tupanie kumfurahisha Bwana.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment