MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 10, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 5 LA MWAKA
SOMO
1
Mwa.
2:4 – 9, 15 – 17
Siku
ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi hapakuwa na mche wa kondeni bado,
wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyesha nchi
mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; ukungu ukapanda katika nchi, ukatia
maji juu ya uso wote wa ardhi. Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,
Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu
akawa nafsi hai.
Bwana
Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo
mtu aliyemfanya. Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa
macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi
wa mema na mabaya. Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya
Edeni, ailime na kuitunza. Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya
kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na
mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
104:1 – 2, 27 – 30 (K) 1
(K)
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Ee
nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Wewe,
Bwana, Mungu wangu,
Umejifanya
mkuu sana;
Umejivika
heshima na adhama.
Umejivika
nuru kama vazi;
Umezitandika
mbingu kama pazia; (K)
Hao
wote wanakungoja Wewe,
Uwape
chakula chao kwa wakati wake.
Wewe
huwapa,
Wao
wanakiokota;
Wewe
waukunjua mkono wako,
Wao
wanashiba mema; (K)
Wewe
wauficha uso wako,
Wao
wanafadhaika;
Waiondoa
pumzi yao, wanakufa,
Na
kuyarudia mavumbi yao,
Waipeleka
roho yako, wanaumbwa,
Nawe
waufanya upya uso wan chi. (K)
SHANGILIO
Zab.
19:8
Aleluya,
aleluya,
Amri
ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.
INJILI
Mk.
7:14 – 23
Yesu
aliwaita makutano tena, akawaambia, NIsikieni nyote na kufahamu. Hakuna kitu
kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile
vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu. Mtu akiwa na masikio ya
kusikilia, na asikie.
Hata
alipoingia nyumbani, ameuacha mkutano, wanafunzi wake wakamwuliza habari za ule
mfano. Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu
kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu
hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema
hivi alivitakasa vyakula vyote. Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho
unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano,
kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment