MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 4, 2021
ALHAMISI
JUMA LA 4 LA MWAKA
SOMO
1
Ebr.
12:18-19, 21-24
Ndugu
zangu hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na
giza na giza, na tufani, na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale
walioisikia walisihi wasiambiwe neno lolote linguine. Na hayo yalionekana jinsi
yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka.
Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa
mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa
wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu
wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya
kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
48:1-2, 8-10 (K) 9
(K)
Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu, katikati ya hekalu lako.
Bwana
ndiye aliye mkuu,
Na
mwenye kusifiwa sana,
Katika
mji wa Mungu wetu.
Katika
mlima wake mtakatifu.
Kuinuka
kwake ni mzuri sana,
Ni
furaha ya dunia yote. (K)
Mlima
Sayuni pande za kaskazini,
Mji wa
mfalme mkuu.
Mungu
katika majumba yake
Amejijulisha
kuwa ngome. (K)
Kama
tulivyosikia, ndivyo tulivyoona,
Katika
mji wa Bwana wa majeshi,
Mji
wa Mungu wetu,
Mungu
ataufanya imara hata milele. (K)
Tumezitafakari
fadhili zako, Ee Mungu,
Katikati
ya hekalu lako.
Kama
lilivyo jina lako, Ee Mungu,
Ndivyo
na sifa yako hata miisho ya dunia,
Mkono
wako wa kuume umejaa haki. (K)
SHANGILIO
Zab.
147:12,15
Aleluya,
aleluya,
Msifu
Bwana, Ee Yerusalemu, huipeleka amri yake juu ya nchi.
Aleluya.
INJILI
Mk.
6:7-13
Siku
ile Yesu aliwaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri
juu ya pepo wachafu; akawakataza wasichukue kitu cha njiani isipokuwa fimbo tu;
wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni; lakini wajifungie viatu, akasema,
Msivae kanzu mbili. Akawaambia, Mahali popote mtakapoingia katika nyumba, kaeni
humo hata mtakapotoka mahali pale. Na mahali popote wasipowakaribisha ninyi
wala kuwasikia, mtokapo huko, yakung’uteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu,
kuwa ushuhuda kwao. Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu. Wakatoa pepo wengi,
wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment