MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 3, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 4 LA MWAKA
SOMO
1
Ebr.
12;4 – 7, 11 – 15
Hamjafanya
vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi. Tena mmeyasahau yale maonyo,
yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana,
wala usizimie moyo ukikemewa naye; maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi,
naye humpiga kil amwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimi; Mungu
awatendea kama wana; maana ni mwana yupi aisyerudiwa na babaye?
Kila
adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini
baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye Amani. Kwa hiyo
inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, mkaifanyie miguu yenu njia
za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kipnywe.
Tafuteni
kwa bidii kuwa na Amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu
atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia kana mtu asiipungukie neema ya
Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi
wakatiwa unajisi kwa hilo.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
103:1 – 2, 13 – 14, 17 – 18
(K)
Fadhili za Bwana zina wamchao tangu milele hata milele
Ee
nafsi yangu, umhimidi Bwana
Naam,
vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi
jina lake takatifu.
Ee
nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Wala
usizisahau fadhili zake zote. (K)
Kama
vile baba awahurumiavyo watoto wake,
Ndivyo
Bwana awahurumia wamchao.
Kwa
maana yeye anatujua umbo letu
Na
kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi. (K)
Fadhili
za Bwana zina wamchao
Tangu
milele na milele,
Na
haki yake ina wana wa wana;
Wale
washikao agano lake. (K)
SHANGILIO
Yn.
8:12
Aleluya,
aleluya,
Mimi
ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, yeye anifuataye hatakwenda gizani na
kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.
INJILI
Mk.
6:1-6
Yesu
alitoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao, wanafunzi wake wakamfuata. Na
ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia
wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, ni hekima gani hii aliyopewa
huyu? Na, ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si
yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na
Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Yesu akawaambia,
Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jaama zake,
na nyumbani mwake. Wala hakuweza kufanya mwujiza wowote huko; isipokuwa aliweka
mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. Akastaajabu kwa sababu ya
kutokuamini kwao.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment