MASOMO YA MISA, FEBRUARI 26, 2021
IJUMAA
YA 1 YA KWARESIMA
SOMO
1
Eze.
18:21-28
Bwana
asema hivi: Mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na
kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki hakika ataishi,
hatakufa. Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo
katika haki yake aliyoitenda ataishi. Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu
mwovu? Asema Bwana Mungu; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake,
akaishi?
Bali
mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya
machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je! Ataishi? Katika matendo yake
yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile
alilolikosa, na katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa. Lakini ninyi mwasema,
Njia ya Bwana si sawa. Sikilizeni sasa, Enyi nyumba ya Israeli; Je! Njia yangu
siyo iliyo sawa? Njia zenu sizo zisizo sawa? Mwenye haki atakapoghairi, na
kuiacha haki yake, na kutenda uovu, atakufa katika uovu huo; katika uovu wake
alioutenda atakufa. Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake
alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki ataponya roho yake, nayo itakuwa
hai. Kwa sababu atafakari, na kughairi, na kuyaacha makosa yake yote
aliyoyatenda, hakika ataishi, hatakufa.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
130 (K) 3
(K)
Bwana kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama?
Ee
Bwana, toka vilindini nimekulilia.
Bwana,
uisikie sauti yangu.
Masikio
yako na yaisikize
Sauti
ya dua zangu. (K)
Bwana,
kama Wewe ungehesabu maovu,
Ee
Bwana, nani angesimama?
Lakini
kwako kuna msamaha,
Ili
Wewe uogopwe. (K)
Nimemgnoja
Bwana, roho yangu imengoja,
Na
neno lake nimelitumainia.
Nafsi
yangu inamngoja Bwana,
Kuliko
walinzi waingojavyo asubuhi,
Naam,
walinzi waingojao asubuhi. (K)
Ee
Israeli, umtarajie Bwana;
Maana
kwa Bwana kuna fadhili,
Na
kwake kuna ukombozi mwingi.
Yeye
atamkomboa Israeli na maovu yake yote. (K)
SHANGILIO
Yoe.
2:12-13
Hata
sasa, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, Asema Bwana, kwa maana mimi ndiye
mwenye neema, Nimejaa huruma.
INJILI
Mt.
5:20-26
Siku
ile Yesu aliwaambia wafuasi wake: Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu
isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kwamwe katika ufalme
wa mbinguni.
Mmesikia
watu wa kale walivyoambiwa, Usiue; na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni,
Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake,
itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanam ya moto.
Basi
ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno
juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na
ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. Patana na mshitaki wako upesi,
wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na
kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. Amin, nakuambia, Hutoki humo
kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
No comments:
Post a Comment