“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kwaresima
Ijumaa,
Februari 26, 2021,
Juma
la 1 la Kwaresima
Eze
18:21-28;
Zab
130: 1-8;
Mt
5:20-26.
KUWA
MWEMA!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo tafakari ya neno
la Bwana tunaanza kwa kuliangalia somo la kwanza ambapo tunamkuta nabii Ezekiel
akituambia kwamba sio Mpango wa Mungu kufurahia kufa kwa mtu mwovu bali auache
mwenendo wake. Hivyo anasema muovu atakayeacha njia yake na kugeuka, huyo
ataponywa na Mungu lakini Mchamungu atakayeiacha njia yake njema na kuasi
atakufa katika uovu wake-asitegemee kwamba ule wema alioutenda mwanzoni
utamuokoa.
Hili
ni fundisho kubwa sana hasa kwa baadhi yetu ndugu zangu. Kuna baadhi yetu
tunafikiri kwamba wakati fulani nilisali sana. Sasa siendi hata kanisani
nikijifariji kwamba zile misa nilizozienda zitaniokoa. Au unakuta baadhi yetu
hatuungami na tunasema nikiwa mdogo niliungama sana, sasa ngoja nitende dhambi
kidogo, ni wakati wa kulipia madhambi. Au wakati mwingine nasema naenda hija
mwaka huu na kusali labda kwa siku tisa halafu kwa kipindi chote cha mwaka
sisali tena. Huku ni kupotoka ndugu zangu na namna hii hatutaweza kumfikia Mungu.
Kama ni wema tuwe wema siku zote. Unapoamua kuwa mwema kwa Mungu, hatuweki
masharti. Unakuwa mwema tangu mwanzo hadi mwisho, usije ukampangia Mungu na
kumwambia kwamba aa, Mungu nilikutii sana pale mwanzoni, acha sasa nitende
dhambi, nipe kapozi kadogo-namna hii siyo. Mungu apenda kitu kikamilifu, na
sisi tumpatie kitu kikamilifu. Kama kweli tumeamua kumtii, basi tumtii siku
zote, tubakie katika muungano naye, sio siku moja nasema-aa, leo natenda
kadhambi kadogo bwana=hapa hatujampenda Mungu, hapa bado tutakuwa tunamkosea
Mungu. Tulio na tabia hizi tuache. Tunaosema-ati leo ni sikukuu, ngoja nilewe
kidogo-sio namna nzuri. Kwa Mungu hakuna siku iliyo ya mlegezo legezo.
Injili
tunamkuta Yesu akiendeleza maada hii kwamba uaminifu ni kubakia katika
muunganiko na Bwana siku zote. Sio kulegeza legeza. Yeye anawaambia kwamba wale
wafarisayo walikuwa na hali ya kulegeza legeza uzito wa amri za Mungu. mfano,
unakuta Mfarisayo anapeleka sadaka hekaluni halafu kumbe hajapatana na ndugu
yake, Mfarisayo anajidai kutamka amri ya tano ya Mungu usiue na kumbe moyoni
anakuangalia kwa hasira. Yesu anawaeleza wanafunzi wake kwamba wasiige mfano
kama huu kwa sababu wao walikuwa hawafanyi kitu kikamilifu mpaka mwisho. Yesu
anawaeleza kwamba kama mtu anakubaliana na amri ya Mungu kwamba usiue, basi
ajue kwamba amri hii inakupasa umpende jirani yako kuliko vyote-hata
kumwangalia vibaya usimwangalie. Usimseme. Huku ndiko kuishika amri. Yeye
anashangaa kuona wafarisayo wanasema usiue lakini bado wanachuki na watu
moyoni. Ndio maana Yesu anawaambia wanafunzi wake haki yao iwazidi ya
wafarisayo-yaaani kama ni kutimiza sheria za Mungu-wasiweke kamlegezo hata siku
moja.
Somo
hili ndugu zangu ni funzo kwetu sisi ambao mara nyingi tayari tumeshaandaa
namna za kujitetea na kufanya na kuhalalisha ili kutenda dhambi. Mwingine
anasema nafanya maramoja tu sitarudia! Hii mara moja sio dhambi? Anayempenda
Mungu hatarusuhu kutenda dhambi hata mara moja. Unakuta mtu anasema-nalewa tu
kwa leo, hakuna kitu kama hicho-mpende Mungu siku zote, unakuta mtu anasema-aah
kwa sababu nimetukana au kufanya uzinzi kwa mara ya kwanza sio dhambi-hakuna
kitu kama hicho. Vyote ni dhambi. Dhambi haina cha ya kwanza na ya mwisho. Zote
ni hatari. Hali ya kusema dhambi za mara ya kwanza sio dhambi au sio nzito
tuache-tuogope dhambi kila wakati.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment