MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 24, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 1 LA KWARESIMA
SOMO
1
Yon.
3:1-10
Neno
la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule
mkubwa, ukaihubiri habari nitakayokuamuru.
Basi
Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikiuwa mji
mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu, Yona akaanza kuuingia mji mwendo
wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi
utaangamizwa.
Basi
watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za
magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Habari ikamfikia mfalme wa
Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika
nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari
katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema. Mwanadamu
asionje kitu, wala mnyama wala makundi ya ng’ombe, wala makundi ya kondoo;
wasile, wala wasinywe maji; bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na
mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache
njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu
hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili tusiangamizwe?
Mungu
akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi
neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
51:1-2, 10-11, 16-17 (K) 17
(K)
Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau.
Ee
Mungu, unirehemu,
Sawa
na fadhili wako.
Kiasi
cha wingi wa rehema zako,
Uyafute
makosa yangu. (K)
Ee
Mungu, uniumbie moyo safi,
Uifanye
upya roho iliyotulia ndani yangu.
Usinitenge
na uso wako,
Wala
roho yako mtakatifu usiniondolee. (K)
Maana
hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa,
Wewe
huridhii sadaka ya kuteketezwa.
Dhabihu
za Mungu ni roho iliyovunjika,
Moyo
uliyovunjika na kupondeka. (K)
SHANGILIO
Eze.
18:31
Tupilieni
mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosea, Asema Bwana. Jifanyeni moyo mpya na
roho mpya.
INJILI
Lk.
11:29-32
Makutano
walipokuwa wakimkusanyikia, Yesu alianza kusema, Kizazi hiki ni kizazi kibaya;
kinatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya Yona. Maana, kama vile
Yona alivyokuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu kwa
kizazi hiki. Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi
hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka nchi za
dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani. Watu wa
Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa
na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa
kuliko Yona.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment