ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya Kwaresima
Jumatano,
Februari 24, 2021.
Juma
la 1 la Kwaresima
Yon
3:1-10;
Zab
51:3-4,12-13,18-19;
Lk
11:29-32
KUMKUBALI
YESU NA UPENDO WAKE!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana
linatupatia ujumbe muhimu kabisa wa kutuongoza katika kipindi chetu cha
Kwaresima. Na neno hili tutaanza kwa kuuangalia wimbo wa katikati ambapo
tunakutana na ujumbe kwamba moyo uliovunjika na kupondeka ee Mungu hutaudharau.
Hii ni Zaburi aliyoiimba Daudi akiwa katika unyenyekevu mkubwa na hali ya
kujiona mnyonge baada ya kutenda kosa la uzinzi na uuaji-kumuua Uriah na
kumchukua mkewe. Aliisali katika moyo wa kupondeka na unyenyekevu mkubwa na hii
ilimsaidia kupokea msamaha toka kwa Mungu na kubarikiwa tena. Nabii Yona katika
somo la kwanza alikuja miaka mia sita baada ya maneno haya kusemwa na Daudi na
yeye sasa katika somo la kwanza anawashauri watu wa Ninawi wajivike moyo
uliovunjika na kupondeka kama alivyojivika Daudi ili wapate msamaha toka kwa
Mungu la sivyo wataangamizwa. Watu wa Ninawi walikubali ujumbe huu na tunasikia
kwamba walijivika moyo uliovunjika na kupondeka na mwishowe walihurumiwa. Yesu,
katika injili anakuja miaka karibu mia nne baada ya Yona kusema maneno haya kwa
watu wa Ninawi na katika Injili Yesu anawaeleza Wafarisayo kwamba hawatapewa
ishara nyingine isipokuwa ile ya Yona.-ishara ya Yona ni ishara ya majuto,
ishara inayonitaka nijione kwamba mimi ni mkosefu nihitajiye neema ya Mungu,
ishara initakayo nikazane niupiganie wokovu wangu, ishara initakayo nijivike
moyo wa kuvunjika na kupondeka kama walivyojivika wale watu wa ninawi na kama
alivyojivika Daudi na kusamehewa. Walipofanya hivi walipata matunda makubwa
maishani mwao lakini Wafarisayo watakapokataa kufanya hivi basi watapatwa na
matatizo mengi na kuukosa wokovu maishani mwao.
Mtazamo
huu ndugu zangu ndio unaonifaa mimi na wewe kwa kipindi hiki. Lazima niende
mbele za Mungu, nikiwa na moyo uliovunjika na kupondeka, moyo wa majuto na
kuomba msamaha na kwa namna hii nitaweza kuona nguvu ya Mungu maishani
mwangu-na kukifanya kipindi hiki kiwe cha faida kwangu. Tuombe msamaha kwa wale
tuliowakosea, tutumie sakramenti ya kitubio vizuri. Dunia inapata shida kubwa
kwa sababu watu hatujioni kama wadhambi, tunajiona kwamba ni wema-na dunia
inalaaniwa kila siku. Tutakapojiona kwamba sisi ni wadhambi, dunia yetu
itabarikiwa tena-familia na jumuiya yangu itabarikiwa tena. Na magomvi
yatapungua. Tumsifu Yesu Kristo
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment