MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 23, 2021
JUMANNE
YA 1 YA KWARESIMA
SOMO
1
Isa.
55:10-11
Bwana
asema: Kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi
huko: bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza ikampa mtu apandaye
mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika
kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo
litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
34:3-6, 15-18 (K)17
(K)
Wenye haki, Bwana anawaponya na taabu zao zote.
Mtukuzeni
Bwana pamoja nami,
Na
tuliadhimishe jina lake pamoja.
Nalimtafuta
Bwana akanijibu,
Akaniponya
na hofu zangu zote. (K)
Wakamwelekea
macho wakatiwa nuru,
Wala
nyuso zao hazitaona haya.
Maskini
huyu aliita, Bwana akasikia,
Akamwokoa
na taabu zake zote. (K)
Macho
ya Bwana huwaelekea wenye haki,
Na
masikio yaje hukielekea kilio chao.
Uso
wa Bwana ni juu ya watenda mabaya,
Aliondoa
kumbukumbu lao duniani. (K)
Walilia,
naye Bwana akasikia,
Akawaponya
na taabu zao zote.
Bwana
yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na
waliopondeka roho huwaokoa. (K)
SHANGILIO
Zab.
95:8
Leo
msifanye migumu mioyo yenu, lakini msikie sauti yake Bwana.
INJILI
Mt.
6:7-15
Siku
ile Yesu aliwaambia wafuasi wake: Mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama
watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu maneno yao
kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla
ninyi hamjamwomba. Basi ninyi salini hivi:
Baba
yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako
yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe
deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni,
lakini utuokoe na yule mwovu.
Kwa
maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa
yenu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment