“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya Kwaresima
Jumanne,
Februari 23, 2021
Juma
la 1 la Kwaresima
Isa
55:10-11;
Zab
34: 4-7, 16-19;
Mt
6: 7-15
KUJIFUNZA
KUSAMEHE!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu siku ya leo. Leo neno la Bwana
tutaanza kwa kuliangalia somo la Injili ambapo tunakutana na Yesu akitufundisha
namna ya kusali. Anatueleza kwamba sala ni tendo takatifu ambalo kwa hilo
tunaungana na Mungu. Ndiyo njia tu mwanadamu anaweza kuongea na Mungu. Na njia
hii ni muhimu. Wapo watu wengi sana wameitumia na wamefanikiwa vizuri kabisa.
Kwa
njia ya sala watu kama akina mtakatifu Fransiko wa Assis waliona maono
makubwa-watu wamefanya miujiza mikubwa na wamepata miujiza maishani mwao kwa
njia ya sala. Kwa kweli hata wewe mwenyewe kuna mahali inafikaga unajiona
unafaulu katika baadhi ya mambo-lakini ukijaribu kujiuliza kwa undani utaona
kwamba hapa pana mkono wa Mungu. Sio kwa nguvu zangu. Huu ni muujiza. Kila mtu
ana stori yake ya kuelezea.
Ndugu
zangu, lakini cha ajabu ni kwamba, licha ya ukweli kwamba sala ina nguvu nyingi
kiasi hicho, watu wanaichezeaga sala na katika Injili Yesu anasema kwamba watu
wanasali kwa kupayuka-bila kutafakari, kwa kujionyesha ili waogopwe na watu na
wapewe sifa na watu. Yesu anapinga kuchezea sala namna hii. Yeye anafundisha
sala na namna ya kusali na anasema kwamba ukianza kusali-kwanza anza kwa
kumtukuza Mungu, yaani unatambua ukuu wake, halafu omba ili aendelee kukubali
kuiongoza dunia-aitawale na mapenzi yake yaenee kila mahali na si mapenzi ya
muovu. Halafu tumweleze shida zetu hasa juu ya mahitaji yetu kama chakula na
kumwomba atusamehe dhambi zetu na asituingize katika majaribu. Sala hii
yahitaji tafakari na haina mahali popote inaposisitiza kwamba mtu ajitukuze
mwenyewe au atumie sala kwa kutishia watu. Namna hii sala huwa takatifu na Mungu
hutusikia.
Katika
somo la kwanza, Mungu anasisitza kwamba maneno yake na mipango yake si mchezo.
Kila asemacho hatanii na mipango yake na neno lake lazima litekeleze ile kazi
iliyotumwa kutekeleza kama mvua iinyeshayo ardhi na ardhi kuchipua.
Huu
ujumbe twaweza kuutafakari unamaanisha kwamba tujue Mungu ni tofauti na sisi na
pale unapotaka kuongea naye au kufanya agano naye au kutaka kusali, jua kwamba
unaongea na ngazi ya juu-usifanye mchezo. Kama ni kwenye sala tuwe makini.
Kwenye sala unaingia katika mazungumzo na Mungu, unapanga naye mipango, lazima
kuwa makini sana tusije tukafikiri kwamba tunapanga mipango ya hivihivi tu.
Masomo
yote haya yanatupatia ujumbe mkuu sana kwaresma hii. Yanatuambia juu ya
kuheshimu sala. Sala si kujionyesha. Waweza kuja kusali ukaishia kulaaniwa
kwani unaishia kwenye kumkufuru Mungu, au kujisifu mwenyewe kama yule Farisayo.
Tuwe na mipango-nikija kanisani niwe na nia, nisali-nimpe Mungu utukufu na mimi
nipate baraka
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment