MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 22, 2021
JUMATATU,
JUMA LA 1 LA KWARESIMA
SOMO
1
Law.
19:1-2, 11-18
Bwana
akanena na Musa, akamwambia, Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie,
Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu.
Msiibe,
wala msidanganye, wala msiambiane uongo. Msiape uongo kwa jina langu, hata
ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi Bwana. Usimdhulumu jirani yako, wala
kumnyang’anya mali yake; ijara yake aliyeajiriwa isikae kwako usiku kucha hata
asubuhi. Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu
wako; Mimi ndimi Bwana. Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu
maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.
Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame
kinyume cha damu ya jirani yako; Mimi ndimi Bwana. Usimchukie ndigu yako moyoni
mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake.
Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende
jirani yako nafsi yako; Mimi ndimi Bwana.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
19:7-9, 14 (K) Yn. 6:64
(K)
Bwana unayo maneno ya uzima wa milele.
Sheria
ya Bwana ni kamilifu,
Huiburudisha
nafsi.
Ushuhuda
wa Bwana ni amini,
Humtia
mjinga hekima. (K)
Maagizo
ya Bwana ni ya adili,
Huufurahisha
moyo.
Amri
ya Bwana ni safi,
Huyatia
macho nuru. (K)
Kicho
cha Bwana ni kitakatifu,
Kinadumu
milele,
Hukumu
za Bwana ni kweli,
Zina
haki kabisa. (K)
Maneno
ya kinywa changu,
Na
mawazo ya moyo wangu,
Yapate
kibali mbele zake, Ee Bwana,
Mwamba
wangu, na mwokozi wangu. (K)
SHANGILIO
Zab.
51:1-10, 12
Ee
Mungu, uniumbie mioyo yenu; Unirudishie furaha ya wokovu wako.
INJILI
Mt.
25:31-46
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake,
na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha
utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama
vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kodnoo mkono wake wa kuume,
na mbuzi mkono wake wa kushoto.
Kisha
Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba
yangu, urithini ufalme, mliowekewa tayari tangu kuubwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa
na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni,
mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama;
nalikuwa kifungoni, mkanijia.
Ndipo
wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa,
tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni,
tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin,
nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo,
mlinitendea mimi.
Kisha
atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa,
mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; kwa
maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa na
kifungoni, msije kunitazama.
Ndipo
hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una
kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye
atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao
walio wadogo, hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu
ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment