MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 20, 2021
JUMAMOSI
BAADA YA MAJIVU
SOMO
1
Isa.
58:9b-14
Bwana
asema hivi: Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala
kunena maovu; na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha
nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako
kitakuwa kama adhuhuri.
Naye
Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na
kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama
chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
Na
watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi
vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye
kurejeza njia za kukalia.
Kama
ukigeuza mguu wako usiihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu
wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima;
ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo
wala kusema maneno yako mwenyewe; ndipo utakapojifurahisha katika Bwana; nami
nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba
yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
86:1-2, 3-4, 5-6 (K) 11
(K)
Ee Bwana, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako.
Ee
Bwana, utege sikio lako unijibu,
Maana
mimi ni maskini na mhitaji,
Unihifadhi
nafsi yangu,
Maana
mimi ni mcha Mungu.
Wewe
uliye Mungu wangu,
Umwokoe
mtumishi wako anayekutumaini. (K)
Wewe,
Bwana, unifadhili,
Maana
nakulilia Wewe mchana kutwa.
Uifurahishe
nafsi ya mtumishi wako,
Maana
nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana. (K)
Kwa
maana Wewe, Bwana, U mwema,
Umekuwa
tayari kusamehe,
Na
mwingi wa fadhili,
Kw
awatu wote wakuitao.
Ee
Bwana, uyasikie maombi yangu;
Uisikilize
sauti ya dua zangu. (K)
SHANGILIO
Eze.
33:11
Waambie,
kama mimi niishivyo, asema Bwana Mungu, Sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; Bali
aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake akaishi.
INJILI
Lk.
5:27-32
Siku
ile: Yesu akaona mtoza ushuru, jina lake Lawi, ameketi forodhani, akamwambia,
Nifuate. Akaacha vyote, akaondoka, akamfuata.
Na
Lawi akamfanyia karamu kubwa nyumbani mwake; palikuwa na mkutano mkuu wa watoza
ushuru na watu wengineo waliokuwa wameketi chakulani pamoja nao. Ikawa
Mafarisayo na waandishi wao kuwanung’unukia wanafunzi wake, wakisema, Mbona
mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? Yesu akajibu
akawaambia, Wenye afya hawana haja na tabibu, isipokuwa walio hawawezi. Sikuja
kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment