MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 2, 2021
JUMANNE,
JUMA LA 4 LA MWAKA
SIKUKUU
YA KUTOLEWA BWANA HEKALUNI
SOMO
1
Mal.
3:1-4
Bwana
Mungu asema hivi: Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia
mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam yule
mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi.
Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama
atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha,
ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na
kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha;
nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki. Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na
Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na kama
katika miaka ya zamani.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
ZAB.
24:7-10 (K) 8
(K)
Ni nani Mfalme wa utukufu? Ni Bwana.
Inueni
vichwa vyenu, enyi malango,
Inukeni,
enyi malango ya milele,
Mfalme
wa utukufu apate kuingia. (K)
Ni
nani Mfalme wa utukufu?
Bwana
mwenye nguvu, hodari,
Bwana
hodari wa vita. (K)
Inueni
vichwa vyenu, enyi malango,
Naam,
viinueni, enyi malango ya milele
Mfalme
wa utukufu apate kuingia. (K)
Ni
nani huyu Mfalme wa utukufu?
Bwana
wa majeshi,
Yeye
ndiye Mfalme wa utukufu. (K)
SOMO
2
Ebr.
2:14-18
Basi,
kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki
yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti,
yaani, Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya
mauti walikuwa katika hali ya utumwa. Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika,
ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake
katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo
ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Na kwa kuwa mwenyewe
aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Lk.
2:32
Aleluya,
aleluya!
Nuru
ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.
Aleluya!
INJILI
Lk.
2:22-40
Zilipotimia
siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa, wazee wa Yesu walikwenda
naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana, (kama ilivyoandikwa katika sheria ya
Bwana, Kila mtoto mwanamume aliye kifungua mimba ya mamaye na aitwe mtakatifu
kwa Bwana), wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Huwa
wawili au makinda ya njiwa wawili. Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu,
jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya
Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. Naye alikuwa ameonywa na Roho
Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. Basi akaja
hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili
wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, yeye mwenyewe alimpokea mkononi
mwake, akamshukuru Mungu, akisema,
Sasa,
Bwana, wamruhusu mtumishi wako, kwa amani, kama ulivyosema; kwa kuwa macho
yangu yameuona wokovu wako, uliouweka tayari machoni pa watu wote; nuru ya kuwa
mwangaza wa mataifa, na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment