“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumanne
, Februari 2, 2021,
Juma
la 3 la Mwaka wa Kanisa
Sherehe
ya Kutolewa Bwana hekaluni.
Mal
3: 1-4;
Zab
24: 7-10;
Ebr
2: 14-18
Lk
2: 22-40.
KUJIWEKA
WAKFU KWA BWANA!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo tunaadhimisha
siku ya kutolewa Bwana hekaluni. Hii ilikuwa ni desturi katika tamaduni za
Kiyahudi kwamba mtoto wa kiume aliyekifungua mimba lazima aitwe mtakatifu wa
Bwana. Anatolewa ili awe mali ya Bwana, awe chombo cha Bwana, amtumikie Bwana
na si shetani. Hadi leo katika kanisa wazo hili linapendelewa sana na hadi leo
tunashuhudia watawa wakijitolea mbele ya Bwana na leo ni siku yao. Wao huiga
mfano wa Yesu, kuyatolea maisha yao kwa ajili ya Bwana na kufanya kazi yake.
Hivyo, leo tuwaombee watawa wetu ambao kwa kweli wamechagua kufuata wazo na
fungu jema. Nasi ndugu zangu, tunaalikwa kuyatolea maisha yetu yote kwa ajili
ya Bwana. Haya ndiyo mawazo makuu yanayotuongoza katika siku ya leo ndugu
zangu.
Na
tukianza kwa kuyachunguza masomo yetu ya leo, tunaona wazo hili la kuwekwa
wakfu, wazo la kutakaswa limejitokeza vizuri kabisa. Somo la kwanza linatoka
katika kitabu cha nabii Malaki ambaye analijia hekalu. Cha ajabu ni kwamba
mjumbe huyu anapofika, sio kwamba hekalu linamtakasa bali ni hekalu lenyewe
linapata kutakasika na dhabihu zinazokuwa zinatolewa pale zinatakaswa na
kupatiwa ubora zaidi. Katika Injili, tunagundua kwamba mjumbe huyu sasa
amekwisha zaliwa, ambaye ndiye Yesu na leo sasa anapelekwa hakaluni kutakaswa.
Na anapofika hekaluni, hakalu linapata baraka badala ya hekalu kumpatia Baraka.
Zile sadaka zinazokuwa zikitolewa hakaluni zinapatiwa ubora, Mungu mwenyewe
anazipatia kiwango, furaha inazidi kwa Mungu kuja hekaluni, na dunia yote
inabarikiwa. Hekalu lenyewe linawekwa wakfu. Katika somo la pili tunasikia
kwamba Yesu analiweka wakfu, sio hekalu peke yake bali amekuja kuwaweka wakfu
watu wote, watu wote kabisa, wanaomwamini kwa damu yake sasa wanakombolewa.
Ndugu
zangu, ndivyo ilivyo kwa siku ya leo. Leo tunaambiwa kwamba Yesu amekwisha
kufika. Ujio wake tu tayari umetutia wakfu. Anapofika hekaluni, hekalu
halimweki wakfu bali yeye ndiye analiweka . Sasa, anapofika kwetu, vivyo hivyo
anatuweka wakfu kwa njia ya sakramenti mbalimbali. Basi, tuishi kama tuliowekwa
wakfu. Tuachane na kuitumia miili yetu vibaya, tuwasaidie na wengine waweze
kujitoa wakfu kwa Bwana. Ukimuona mwenzako anakataa kuishi utakatifu, msaidie,
usimletee vishawishi au kumshauri vibaya.
Tujue
kwamba ni dhambi kubwa kumfanya mwenzako anayetaka kujiweka wakfu aidha kwa
kuishi kiaminifu ndoa yake au utawa wake, sasa wewe unamdanganya asiiishi
kiwakfu. Kama umeshafanya hivyo ungama. Popote pale ambapo umewahi kumfanya
mwenzako ashindwe kuishi kiwakfu, asiyaishi maisha yake kitakatifu
tujirekebishe.
Kuwashawishi
watu waliojiweka wakfu aidha kwa ndoa takatifu au utawa na kuwadumbukiza ufanye
nao dhambi au kwa kushirikiana nao na wewe ukawapeleka katika dhambi kama
kushiriki katika rushwa Fulani, ukawafundisha uzinzi, jua ni dhambi kubwa. Ni
kama mtu mwenye kuikufuru madhabahu ya Bwana. Hivyo, tuwe makini. Ogopa kitu
kilichotolewa wakfu kwa Bwana. Kitakulaani maisha yako yote.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment