MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 18, 2021
ALHAMISI
BAADA YA MAJIVU
SOMO
1
Kum.
30:15-20
Musa
aliwaambia watu akisema: Aangalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na
mauti na mabaya; kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana, Mungu wako, kuenenda
katika njia zake, na kushika maagizo yake, na amri zake, na hukumu zake, upate
kuwa hai na kuongezeka; Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika nchi
uingiayo kuimiliki. Lakini moyo wako ukikengeuka, usipotaka kusikiza, lakini
ukavutwa kando kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia; nawahubiri hivi
leo hakika mtaangamia; hamtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi, uivukiayo
Yoradani, uingie kuimiliki. Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo,
kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti Baraka na laana; basi chagua uzima,
ili uwe hai, wewe na uzao wako; kupenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake,
na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako, na wingi wa siku zako; upate
kukaa katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako, Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo,
kuwa atawapa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
1:1-4, 6 (K) Zab. 39:5
(K)
Heri mtu aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake.
Heri
mtu yule asiyekwenda
Katika
shauri la wasio haki;
Wala
hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala
hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Bali
sheria ya Bwana ndiyo impendezayo,
Na
sheria yake huitafakari mchana na usiku. (K)
Naye
atakuwa kama mti ulipopandwa
Kandokando
ya vijito vya maji,
Uzaao
matunda yake kwa majira yake,
Wala
jani lake halinyauki;
Na
kila alitendalo litafanikiwa. (K)
Sivyo
walivyo wasio haki;
Hao
ni kama makapi yapeperushayo na upepo.
Kwa
kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki,
Bali
njia ya wasio haki itapotea. (K)
SHANGILIO
Zab.
130:5
Nimemgnoja
Bwana, roho yangu imengoja, na neno lake nimelitumaini. Nafsi yangu inamngoja
Bwana, kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, naam, walinzi waingojao asubuhi.
INJILI
Lk.
9:22-25
Siku
ile: Yesu aliwaambia wafuasi wake kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso
mengi na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na
siku ya tatu kufufuka.
Akawaambia
wote, Mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake
kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na
mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Kwa
kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, na kujipoteza
mwenyewe?
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment