ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kwaresima
Alhamisi,
Febrauri 18, 2021,
Alhamisi
baada ya Jumatano ya majivu
Kum
30: 15-20;
Za
1: 1-4, 6;
Lk
9: 22-25
KUIPATA
ROHO KWA KUPOTEZA ULIMWENGU!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo neno la Bwana
katika asubuhi ya leo tunaanza kwa kuingalia injili yetu ambapo tunakutana na
Yesu akiwaeleza wanafunzi wake juu ya mateso ambayo yeye kama Masiha
angeyapokea huko Yerusalem. Habari hizi hizi zilikuja kwao kwa mshtuko mkubwa
na walizipokea kwa huzuni. Hii ni kwa sababu zilikuwa kinyume cha matarajio
yao; wengi kati yao walikuwa hawategemei kitu kama Masiha wao angeingia katika
mateso makali hivi. Hii iliwashtusha kwa sababu nao walitambua kwamba Bwana wao
akipata mateso basi na wao watayapata, itawabidi nao wabebe msalaba uliobebwa
na Bwana wao. Hivyo, waliona kwamba walikuwa wanakwenda kuishia maisha ya
shida. Lakini Yesu alizidi kuchukuliana nao hivyo hivyo taratibu na kuwaongoza
taratibu hadi walipokwisha kutambua nini umuhimu wa msalaba na cha kushangaza
ni kwamba baada ya Yesu kuwapa Roho Mtakatifu, walikuja kuona kwamba mateso ni
kitu kidogo tu. Hivyo walikuwa tayari kuteseka, kuchapwa viboko, kufungwa na
hata kufa kifo dini. Lakini ukiambiwa walikoanzia, kulikuwa mbali.
Ndivyo
na sisi ndugu zangu, pengine wengine tumeingia maisha ya ndoa au ya utawa
tukiwa na malengo tofauti. Tulifikiri kwamba baadhi yetu tumefaidi, tungekuwa
na raha, hakutakuwa na mateso na labda leo nina misukosuko, ninakabiliana na
umaskini, ndoa inasumbua, mume au mke hanisikilizi, utawa hauendi, mambo ni
magumu kila wakati, sijisikii ile raha. Injili yetu ya leo inatuambia kwamba
mitume nao walikutana na hali kama hii. Walijiona kupotea-lakini walipopokea
Roho Mtakatifu, walijiona kwamba wapo mahali sahihi na hawakutaka watoke pale
walipokuwapo bali walikuwa tayari kupata kifo dini pale.
Katika
somo la kwanza, Musa anawaambia wana wa Israeli wachague kati ya kifo au uzima.
Na anawaeleza kwamba endapo watachagua njia ya kifo, hakika atawaangamiza, na
anaapa kabisa kwamba atawaangamiza. Njia ya kifo siku zote inakuwaga rahisi
rahisi, inakataa mateso. Lakini inaongoza motoni. Sisi tunaonyeshwa na Yesu leo
kwamba kuubeba msalaba, kupitia ile njia aliyopitia mkombozi wetu, ndio njia
iongozayo kwenye uzima ambako tunakusikia katika somo la kwanza.
Masomo
yetu haya ni onyo kwetu hasa kwa wale walioishia kuwakimbia wake au waume zao
kutokana na umaskini au ugonjwa. Nawambia hapa mmechagua njia ya kifo. Wale
mliotelekeza watoto wenu walipopata magonjwa au binti apatapo mimba wewe
unamkana au hata kama umewahi kumkana mtu yeyote ili ujiepushie na aibu. Hapa
tulidumbukia katika kuchagua njia ya kifo, njia rahisi. Ni wakati wa kuomba
msamaha kwa Mungu leo.
Shukrani
za pekee ziwafikie nyie mliosafiri na wake au waume zenu katika ugonjwa au
umaskini bila kuwatelekeza, wale mliokubali kubeba misalaba ya wenzenu,
mlioachiwa watoto na mabinti zenu mkalea bila kuwatelekeza au kutupa. Shukrani
sana. Hapa mlichagua njia ya uzima. Tumsifu Yesu Kristo.
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment