MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 15, 2021
JUMATATU,
JUMA LA 6 LA MWAKA
Mwa
4: 1-15, 25;
Adamu
alimjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto
mwanamume kwa Bwana. Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa
mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. Ikawa hatimaye Kaini akaleta
mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa
wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na
sadaka yake; bali Kaini hakumakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika
sana, uso wake ukakunjamana. Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na
kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali?
Usipotenda vyma dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini
yapasa uishinde. Kaini akamwambia Habili nduguye, twende uwandani. Ikawa
walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, akamwua.
Bwana
akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi
wa ndugu yangu? Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia
kutoka katika ardhi. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua
kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi
haitakupa mazao yake; utakuwa mtoto na mtu asiye na kikao duniani. Kaini
akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. Tazama,
umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami
niakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye
ataniua. Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipizwa
kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
Adamu
akamjua mke wake tena; akazaa mwana mwanamume, akamwita jina lake Sethi; maana
alisema, Mungu ameniwekea uzao mwingine mahali pia Habili; kwa sababu Kaini
alimwua.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
50:1, 8, 16 – 17, 20 – 21 (K) 14
(K)
Umtolee Mungu dhabihu za kushukuru.
Mungu,
Mungu Bwana, amenena, ameiita nchi,
Toka
maawio ya jua hata machweo yake.
Sitakukemea
kwa ajili ya dhabihu zako,
Na
kafara zako ziko mbele zangu daima. (K)
Bali
mtu asiye haki, Mungu amwambia,
Una
nini wewe kuitangaza sheria yangu,
Na
kuliweka agano langu kinywani mwako?
Maana
wewe umechukia maonyo,
Na
kuyatupa maneno yangu nyuma yako. (K)
Umekaa
na kumsengenya ndugu yako,
Na
mwana wa mama yako umemsingizia.
Ndivyo
ulivyofanya, nami nikanyamaza,
Ukadhani
ya kuwa Mimi ni kama wewe.
Walakini
nitakukemea;
Nitayapanga
hayo mbele ya macho yako. (K)
SHANGILIO
1Sam.
3:9
Aleluya,
aleluya,
Nena,
Bwana, kwa kuwa mtumishi wako anasikia: Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
Aleluya.
INJILI
Mk.
8:11 – 13
Walitokea
Mafarisayo, wakaanza kuhojiana na Yesu; wakitafuta kwake ishara itokayo
mbinguni; wakimjaribu. Akaugua rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki
chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki. Akawaacha
akapanda tena chomboni, akaenda zake hata ng’ambo.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment