MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 13, 2021
JUMAMOSI,
JUMA LA 5 LA MWAKA
SOMO
1
Mwa.
3:9 – 24
Bwana
Mungu alimwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, nalisikia sauti yako
bustanini, naliogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Akasema, Ni nani
aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza
usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa
matunda ya mti huo, nikala. Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili
ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.
Bwana
Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko
wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na
mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo
mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe
utamponda kisigino.
Akamwambia
mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa
watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Akamwambia
Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao
nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaani kwa ajili yako; kwa uchungu
utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia,
nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata
utakapoirudia ardhi, ambayo kaitka hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe,
nawe mavumbini utarudi.
Adamu
akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio
hai. Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. Bwana
Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na
mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima,
akala, akaishi milele; kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni,
ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka
Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka
huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
90:2 – 6, 12 – 13 (K) 1
(K)
Wewe Bwana, umekuwa makao yetu, kizazi baada ya kizazi.
Kabla
haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia
Na
tangu milele hata milele ndiwe Mungu. (K)
Wamrudisha
mtu mavumbini,
Usemapo,
Rudini, enyi wanadamu.
Maana
miaka elfu machoni pako
Ni
kama siku ya jana ikiisha kupita,
Na
kama kesha la usiku. (K)
Wawagharikisha,
huwa kama usingizi,
Asubuhi
huwa kama majani yameayo.
Asubuhi
yachipuka na kumea,
Jioni
yakatika na kukauka. (K)
Utujulishe
kuzihesabu siku zetu,
Tujipatie
moyo wa hekima.
Ee
Bwana, urudi, hata lini?
Uhurumie
watumishi wako. (K)
SHANGILIO
Zab.
25:4, 5
Aleluya,
aleluya,
Ee
Bwana, unijulishe njia zako, unifundishe mapito yako.
Aleluya.
INJILI
Mk.
8:1 – 10
Katika
siku zile, kwa vile ulivyokuwa mkuu tena ule mkutano, nao wamekosa kitu cha
kula, Yesu aliwaita wanafunzi wake, akawaambia, Nawahurumia mkutano kwa sababu
yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula; nami nikiwaaga waende
zao nyumbani kwao hali wanafunga, watazimia njiani; na baadhi yao wametoka
mbali. Wanafunzi wake wakamjibu, Je! Ataweza wapi mtu kuwashibisha hawa mikate
hapa nyikani? Akawauliza, Mnayo mikate mingapi? Wakasema, Saba.
Akawaagiza
mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa
wanafunzi wake waaandikie; wakawaaandikia mkutano. Walikuwa na visamaki
vichache; akavibariki, akasema wawaandikie na hivyo pia. Wakala, wakashiba,
wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba. Na watu waliokula wapata
elfu nne. Akawaaga. Mara akapanda chomboni pamoja na wanafunzi wake, akaenda
pande za Dalmanutha.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment