MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 12, 2021
IJUMAA,
JUMA LA 5 LA MWAKA
SOMO
1
Mwa.
3:1 – 8
Nyoka
alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.
Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti
yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini
twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema,
Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika
hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti
huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Mwanamke
alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa
kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na
mumewe, anaye akala. Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi,
wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Kisha
wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga;
Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
32:1 -2, 5 – 7 (K) 1
(K)
Heri aliyesamehewa dhambi.
Heri
aliyesamehewa dhambi,
Na
kusitiriwa makosa yake.
Heri
Bwana asiyemhesabia upotovu,
Ambaye
rohoni mwake hamna hila. (K)
Nalikujulisha
dhambi yangu,
Wala
sikuuficha upotovu wangu.
Nalisema,
Nitayakiri maasi yangu kwa Bwana,
Nawe
ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu. (K)
Kwa hiyo
kila mtu mtauwa
Akuombe
wakati unapopatikana.
Hakika
maji makuu yafurikapo,
Hayatamfikia
yeye.
Ndiwe
sitara yangu, utanihifadhi na mateso,
Utanizungusha
nyimbo za wokovu. (K)
SHANGILIO
Zab.
119:34
Aleluya,
aleluya,
Unifahamishe
nami nitaishika sheria yako, maajabu yatokayo katika sheria yako.
Aleluya.
INJILI
Mk.
7:31 – 37
Yesu
alitoka katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka bahari
ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli. Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye
utasi, wakamsihi amwekee mikono. Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole
vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, akataama juu mbinguni,
akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka mara masikio yake yakafunguka,
kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri. Akawaonya wasimwambie mtu;
lakini kadiri ya alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari;
wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda mambo yote vema; viziwi
awafanya wasikie, na bubu waseme.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment