"ASALI
ITOKAYO MWAMBANI"
Tafakari
ya kila siku
Ijumaa,
Februari 12, 2021,
Juma
la 5 la mwaka wa Kanisa
Mwa
3: 1-8;
Zab
32: 1-7;
Mk
7: 31-37.
EPHATHA,
FUNGUKA!
Karibuni
sana ndugu zangu wapendwa kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Neno
la Bwana leo linatueleza kwamba wana heri wale waliosamehewa kosa lao,
wasiokuwa na hatia tena, ambao dhambi zao zimeondolewa. Ambao hawahesabiwi kosa
tena na Mungu.
Zaburi
hii inatumika kutilia mkazo kile kisemwacho katika somo la kwanza. Hapa
tunakutana na wazee wetu wakitenda kosa, kosa la kukosa utii, wanakiuka amri ya
Mwenyezi Mungu, wanakuwa na kiburi, wanatafuta madaraka ya kutaka kufanana na
Mungu mwenyewe. Wanataka kujikomboa toka katika mamlaka ya Mwenyezi Mungu. Hili
ni kosa kubwa, kutaka kutwaa madaraka ya Mwenyezi Mungu, kutaka kumpindua Mungu
na kumkosesha madaraka. Mungu aonekane kama sisi, awe mmoja wetu. Ndilo kosa
linalotendeka leo. Mungu atawapa adhabu kali. Lakini basi zaburi yetu
inatuambia kwamba tufurahi kwani hili kosa lilikwishasamehewa kwa Yesu
aliyekufa msalabani.
Hivyo
tuna neema tele, hatuishi tena chini ya laana, tupo na Yesu, tumesamewa kosa.
Shukrani kwa Yesu Kristo. Kwa njia yake tunakila sababu ya kucheka; hakuna haja
ya kilio tena. Tumshukuru Yesu, Yesu ametufundisha kwamba ni lazima kunyenyekea
mbele ya Mungu. Sisi tubakie katika kunyenyekea.
Katika
somo la injili, tunakutana na Yesu akimponya mtu aliyekuwa bubu na kiziwi na
huyu anapona na watu wanafurahi kabisa. Yesu ni sababu yetu sisi kufurahi. Leo
amemtembelea huyu bubu na kiziwi na hakika amepata kusema na kusikia. Sisi
tuombe na Yesu atutembelee leo maishani kama anavyomtembelea huyu mgonjwa wa
leo. Tusikubali Yesu apite pembeni yetu na kutuacha, bila kufanya chochote.
Tumguse
Yesu leo, tumlilie, aje kwetu na atuguse. Hakika tutafaidi kama huyu bubu na
kiziwi anavyofaidi leo. Tumsifu Yesu Kristo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment