“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Ijumaa,
Februari 5, 2021,
Juma
la 4 la Mwaka wa Kanisa
KUMBUKUMBU
YA MT. AGATHA (MSHAHIDI)
Ebr
13: 1-8;
Zab
27: 1, 3, 5, 8-9;
Mk
6: 14-29.
CHAGUA
KULINDA MAISHA!
Ndugu
zangu wapendwa, karibuni kwa tafakari ya neno la Mungu asubuhi ya leo katika
adhimisho la Misa Takatifu. Neno la Bwana leo katika somo la kwanza, mwandishi
wa waraka kwa Waebrania anaanza kuhitimisha kitabu chake kwa kutoa mashauri
mbalimbali.
Anawaeleza
wakristo wake kwamba wawe watu wa kujali, waepukane na tabia ya kutojali.
Watambue kwamba katika jamii kuna watu wenye mahitaji mbalimbali-watambue
kwamba kuna watu tofauti-kuna wagonjwa, wazee, wageni, wengine ni washamba,
wasiojua vitu, kuna vichaa, wengine akili haziko vizuri, wengine wanapata
hasira kiurahisi basi wanapaswa kutambua hilo na kuweza kuishi na kila mmoja
kama rafiki.
Anawaeleza
kwamba Yesu huonekana ndani ya watu kama hawa. Hivyo wajitahidi kuishi na kila
mmoja kwa hekima. Ikikosekana hili hatuwezi kutumikiana ndani ya jamii. Hekima
ndio inayokosekana ndani ya jamii zetu ndugu zangu. Wenzetu hatuwajali kama ni
tofauti, wanahitaji kutendewa tofauti. Kuna wagonjwa labda wa kisukari, wengine
ni vilema-lakini tunataka wale kama sisi, watembee kama sisi, na kila kitu
atende kama sisi. Hapana, watu ni fofauti. Kuna mwingine ni mshamba au
mgeni-amekuja Dar es salaam kwa mara ya kwanza-hawezi kuelewa mji kama wewe.
Akikuuliza kitu usicheke. Wengine wanahamaki haraka au hasira za ajabu-tuishi
nao tukijua hili. Hapa ndipo tunapoweza kumwalika Yesu nyumbani kwetu.
Tukikosa
hekima ya namna hii tutaishia kugombana na wenzetu kila kukicha.
Kwenye
somo la injili, tunakutana na Herode akihofia juu ya Yesu akifikiri kwamba ni
Yohane mbatizaji amefufuka. Pia tunapata maelezo juu ya namna Herode
alivyomkata kichwa Yohane Mbatizaji. Yeye kabla ya kuamuru Yohane akatwe
kichwa-alikuwa katika raha, mwili wake ukisisimka kwa vionjo vya raha
vikamfanya hata kuwa tayari kutoa hukumu iliyokuja kumgharimu kwa maisha yake
yote.
Hii
linatokea kwa sababu kipindi mwili wako ukiwa katika raha, wakati vionjo vyote
vya mwili vikiwa vimeamshwa ndio shetani humkuta karibu. Na hapa tunakamatwa
kirahisi. Dhambi nyingi au maamuzi mabaya hutolewa kwa vipindi kama hivi. Hivyo
tujitahidi kuthibiti vionjo vyetu ndugu zangu ili visitumiwe na shetani.
Kikitokea
kipindi cha furaha, tupambane na vionjo vyake. Tumsifu Yesu Kristo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment