ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Januari
3, 2021.
Sherehe
ya Tokeo la Bwana (Epifania)
Isa
60: 1-6;
Zab
72: 1-2, 7-8, 10-13;
Efe
3: 2-3, 5-6;
Mt
2: 1-12.
ZAWADI
KWA DUNIA NZIMA!
Katika
somo la kwanza, katika ono lake la kinabii, Isaya anaona ujio wa Mungu
ulimwenguni. Utakuja muda ambapo watu wote wataletwa pamoja mbele ya Bwana na
watabarikiwa sana. Utukufu wa Bwana utashuka ulimwenguni na utukufu wake
utauzunguka uumbaji wote.
Tukio
hili takatifu litalibadilisha jiji la Yerusalemu na wale wote wanaofanya kazi
na kuvumilia watapokea mwanga wa uhai.
Katika
somo la pili, Paulo anaifumbua siri ambayo Mungu anaitoa kwa utukufu wake watu
wote pamoja na wapagani, kuwafanya warithi wa ufalme wake. Anasema “sasa
imefunguliwa kuwa wapagani wanashiriki urithi ule ule”. Ukombozi wa ulimwengu,
Mungu pia anawapenda wasio Wakristo kwani wao pia ni wapokeaji.
Leo
tunasherehekea sherehe ya Tokeo la Bwana. Ni sherehe ya dhihirisho la Bwana
wetu kwa watu wa Mataifa. Kulikuwa na mamajusi watatu kutoka mashariki
waliokuja kwa Mfalme mpya aliyezaliwa. Mamajusi hawa, watu wa mataifa, ambao
hawakuwa katika utajiri wa pamoja wa Waisraeli, walikuwa ni watu waliosoma
nyota kwa lengo la kubaini siri na ujumbe wake. Walipokuja katika mahakama ya
mfalme, walimuuliza Herode, yuko wapi mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa?
Hawakuuliza kama mfalme wa wayahudi amezaliwa? Walikuwa na uhakika kuwa mfalme
alikuwa amekwisha zaliwa. Walikuwa tu hawana uhakika wa sehemu yake
alipozaliwa, bali juu ya ukweli kwamba amezaliwa walikuwa nao.
Kama
tu vile Yeye alivyo jidhihirisha Yeye Mwenyewe kwa wale mamajusi, kila siku
Mungu anajidhihirisha mwenyewe kwetu sisi katika Ekaristi Takatifu. Tunamtukuza
Yeye, tunamshukuru na kumfanya yeye afahamike ulimwenguni kote. Basi tujitoe
sisi wenyewe kama zawadi na tuunganike naye na
kuhubiri:Mungu amejidhihirisha mwenyewe duniani. Yesu anajitoa mwenyewe
zawadi kwa dunia nzima.
Sala:
Bwana, niwezeshe niweze kujitoa Mimi mwenyewe kama zawadi kwako. Amina..
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment