MASOMO
YA MISA JANUARI 3, 2021
DOMINIKA
YA TOKEO LA BWANA
SHEREHE
YA EPIFANIA
SOMO
1
Isa.
60:1-6
Ondoka,
ee Yerusalemu, uangaze; Kwa kuwa nuru yako imekuja. Na utukufu wa Bwana
umekuzukia. Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika
kabila za watu; Bali Bwana atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu
yako. Na mataifa wataijilia nuru yako, Na wafalme kuujia mwanga wa kuzuka
kwako. Inua macho yako, utazame pande zote; Wote wanakusanyana; wanakujia wewe;
Wana wako watakuja kutoka mbali, Na binti zako watabebwa nyongani. Ndipo
utakapoona na kutiwa nuru, Na moyo wako utatetemeka na kukunjuka; Kwa kuwa
wingi wa bahari utageuzwa kukujia, Utajiri wa mataifa utakuwasilia. Wingi wa
ngamia utakufunika, Ngamia vijana wa Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka
Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; Na kuzitangaza sifa za Bwana.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
72:1-2, 7-8, 10-13 (K) 11
(K)
Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, ee Bwana.
Ee
Mungu, mpe mfalme hukumu zako.
Na
mwana wa mfalme haki yako.
Atawaamua
watu wako kwa haki,
Na
watu wako walioonewa kwa hukumu. (K)
Siku
zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi,
Na
wingi wa Amani hata mwezi utakapokoma
Na
awe na enzi toka bahari hata bahari,
Toka
mto hata miisho ya dunia. (K)
Wafalme
wa Tarshisi na visiwa walete kodi,
Wafalme
wa Sheba na Seba na watoe vipawa.
Naam,
wafalme wote na wamsujudie;
Na
mataifa yote wamtumikie. (K)
Kwa
maana atamwokoa mhitaji aliapo,
Na
mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi
Atamhurumia
aliye dhaifu na maskini,
Na
nafsi za wahitaji ataziokoa. (K)
SOMO
2
Efe.
3:2-3, 5-6
Ndugu
zangu: Ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili
yenu; ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo.
Siri
hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume
wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; ya kwamba Mataifa ni
warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja
nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Mt.
2:2
Aleluya,
aleluya,
Tuliona
nyota yake mashariki, Nasi tumekuja kumsujudia.
Aleluya.
INJILI
Mt.
2:1-12
Yesu
alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama,
mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, Yuko wapi yeye aliyezaliwa
mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, ansi tumekuja
kumsujudia. Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia
pamoja naye. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta
habari kwao: Kristo azaliwa wapi? Nao wakamwambia, Katika Bethlemu ya Uyahudi;
kwa maana ndiyvo ilivyoandikwa na nabii, Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,
Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda, Kwa kuwa kwako atatoka mtawala
atakayewachunga watu wangu Israeli.
Kisha
Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu
ilipoonekana ile nyota, Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia mkaulize
sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende
nimsujudie. Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile
nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali
alipokuwapo mtoto. Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno.
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka
wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na
uvumba na manemane. Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie
Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment