"ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi,
Januari 7, 2021.
Juma
baada ya Epifania
1
Yoh 4:19 - 5:4;
Zab
72: 1-2, 14-15;
Lk
4: 14-22
*YESU,
MASIHI WETU!*
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo katika somo la
kwanza wazo kuu linalosisitizwa ni kwamba hatuwezi kusema kwamba tunampenda
Mwenyezi Mungu ikiwa hatumpendi mwenzetu tunayemuona mbele ya macho yetu. Hili
linalozungumzwa na Yohane ni kweli.
Mara
nyingi tunatabia ya kujionesha. Tunajidai kwenda kutoa misaada kwa watu wa
mbali wakati wale tunaokaa nao karibu wanahangaika ajabu. Tunatabia ya kutafuta
umaarufu, tunatoa pale tu tunapoonekana. Haya yote ni lazima tujirekebishe,
tabia za namna hii zinawafanya wengi waumie na kutelekezwa.
Tusitegemee
kwamba watu wa mbali watafahamu matatizo ya maskini waliokaribu yetu kuliko
sisi. Sisi ndio tunaofahamu na hakika tuwasaidie. Tupambane pia na tabia za
uvivu-kweli tukishaanza kumsaidia mwenzetu, kuna kasumba ya kuchoka kwa haraka
kutokana na uvivu. Hatuwezi kumsaidia mwenye shida kila siku bila ya kuchoka au
kuanza kumsumanga. Yote haya ni shetani tunayepaswa kupambana naye katika
maisha yetu ya kujitolea. Yanayo turudisha nyuma na vitu kama hivi. Sisi
tupambane navyo.
Katika
injili, Yesu anakataliwa na watu wa kijijini kwake. Sababu zinazotolewa
zinaendana na familia yake-kwamba alitoka familia ya kawaida tu, Baba yake na
Mama yake walifahamika kama watu wasiokuwa na jipya. Hivyo walikataa kumpokea.
Tabia hii iliwafanya wasipate nafasi ya kufanyiwa miujiza toka kwa Yesu kama
ilivyokuwa kwa miji mingine. Halafu hata Yesu hakuchagua mitume wake miongoni
mwa hawa watu wa kijijini mwake.
Ndugu
zangu, Yesu huvutiwa na wanyenyekevu. Hufurahia kukaa mahali ambapo
amekaribishwa na kujisikia nyumbani. Aliamua kujionesha kwa wachungaji kwa
sababu wachungaji walikuwa rahisi kumpokea. Sisi tusiache kuwa wanyenyekevu
mbele ya Yesu. Tujifungue, tumpokee naye atakuja kwetu. Majivuno humfukuza Yesu.
Nasi pia tunaalikwa kuwa na unyenyekevu wa kuweza kumvutia kila mmoja wetu.
Tujiweke kwa namna ambayo kila mmoja wetu anaweza kuja kwetu na kukaribishwa.
Tusijione kuwa mashuhuri sana au wakuu sana kiasi kwamba tunashindwa
kumkaribisha mwenzetu. Tuache tabia hizi. Tumsifu Yesu Kristo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment