MASOMO YA MISA, JANUARI 7, 2021
ALHAMISI
BAADA YA EPIFANIA
SOMO
1
1Yoh.
4:19-5:4
Wapenzi:
Sisi twampenda Mungu kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. Mtu akisema,
Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda
ndugu yake ambaye amemwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye
ampendaye Mungu, ampende ndugu yake.
Kila
mtu aaminiye kwamba Yesu Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye
mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye. Katika hili twajua kwamba twapenda
watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana kila kitu
kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako
ulimwengu, hiyo Imani yetu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
72:1-2, 14-15 (K) 11
(K)
Mataifa yote ya dunia watakusujudia, Ee Bwana.
Ee
Mngu, mpe mfalme hukumu yako,
Na
mwana wa mfalme haki yako.
Atawaamua
watu wako kwa haki,
Na
watu wako walioonewa kwa hukumu. (K)
Atawakomboa
nafsi zao na kuonewa na udahlimu,
Na
damu yao ina thamani machoni pake.
Na
wamwombee daima;
Na
kumbariki mchana kutwa. (K)
Jina
lake na lidumu milele,
Pindi
ling’aapo jua jina lake liwe na wazao;
Mataifa
yote na wajibariki katika yeye,
Na
kumwita heri. (K)
SHANGILIO
Lk.
7:16
Aleluya,
aleluya,
Nabii
mkuu ametokea kwetu; na Mungu amewaangalia watu wake.
Aleluya.
INJILI
Lk.
4:14-22
Siku
ile, Yesu alirudi kwa nguvu za Roho, akaenda Galilaya; habari zake zikaenea
katika nchi zote za kandokando. Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao,
akitukuzwa na watu wote.
Akaenda
Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama
ilivyokuwa desturi yake, akasimama ilia some. Akapewa chuo cha nabii Isaya,
akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu yangu,
kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma
kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha
huru waliosetwa, na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
Akakifunga
chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi
wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni
mwenu.
Wakamshuhudia
wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment