“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumanne
, Januari 26, 2021,
Juma
la 3 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu
ya Watakatifu Timotheo na Tito(Maaskofu)
2
Tim 1: 1-8 au Tit 1: 1-5;
Zab
96: 1-3, 7-8, 10;
Lk
10: 1-9.
WAJUMBE
WA AMANI
Leo
tunaangalia juu ya wazee wetu wa Imani na jinsi walivyo weka Injili katika
matendo yao baada ya ufufuko wa Yesu. Hawa wanaume na wanawake ni wa kizazi cha
pili: wafuasi wa wafuasi na walikuwa wakitumwa mara kwa mara wakiwa wawili
wawili kuhubiri kwa uwepo wao. Kwa njia ya kutembelea na kusafiri inaonyesha kwamba
ufalme wa haki na Amani ulikuwa tayari Ulimwenguni.
Ujumbe
kutoka katika barua kwa Timotheo, Paulo anaelezea mapendo yake makubwa kwa
Timotheo, na wenzake katika utume, na hamu yake kubwa ya kumuona. Anamshukuru
Mungu kwa Imani ya Timotheo alioonesha kwa mama yake Myahudi na bibi yake
Loisi. Wakati huo huo anamkumbusha Timotheo kuhusu zawadi aliopokea wakati
Paulo alivyo mwekea mikono juu yake. Zawadi anayosema Paulo, ilikuwa sio ya
woga bali yenye nguvu, upendo na ujasiri na kuleta ujasiri wote wakuhubiri
Injili hata wakati, wa kipindi cha Paulo, kuonewa na kuteswa. Katika somo la
kuchagua la pili, kutoka katika barua ya Paulo kwa Tito, Paulo anawakumbusha
wamisionari wenzake juu ya kazi ya mtume. Ni “kuwaleta wote ambao Mungu
amewachagua kwenye Imani na akili ya kweli inayo ongoza kwenye dini ya kweli”.
Katika
somo la Injili linaongelea kuhusu maelekezo anayotoa Yesu kwa wale Wafuasi 72
anavyowatuma kwenda kwa utume kufanya kazi ile ile aliokuwa akifanya yeye
mwenyewe. Maneno yake ya ufunguzi ni kweli kama ilivyokuwa katika kipindi cha
Timotheo na Tito: “mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache; hivyo
muombeni Bwana wa mavuno apelike wafanya kazi katika shamba lake.” Ujumbe wao
ulipaswa kuwa wenye kuponya. Sio tuu uponyaji wa mwili tu, bali uponyaji wa
kila aina unaofanya mahusiano na maisha ya watu yalete Amani. Kwa kufanya hivi
walileta uwepo wa ufalme wa Mungu kwa watu walio watembelea. Ni upendo na uwezo
wakuishi kwa pamoja kwa kujaliana na kusaidiana vinaonesha uwepo wa Ufalme wa
Mungu katika maisha yetu. Haya ndio Timotheo na Tito walijitolea kufanya.
Sisi-hata tungekuwa na cheo ghani katika jamii ya Kikristo-tunaitwa kufanya
hayo hayo.
Sala:
Bwana, ninaomba niwe mjumbe wako wa Amani na uponyaji. Ninaomba nijifunze
kutegemea nguvu zako na kuishi maisha nikijikabidhi katika utume wako. Yesu
nakuamini wewe. Amina
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment