MASOMO
YA MISA, JANUARI 26, 2021
JUMANNE,
JUMA LA 3 LA MWAKA
KUMBUKUMBU
YA WATAKATIFU TIMOTHEO NA TITO, MAASKOFU
SOMO
1
2
Tim. 1:1-8
Paulo,
mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa ajili ya ahadi ya uzima ulio
katika Kristo Yesu; kwa Timotheo, mwanangu mpendwa. Neema na iwe kwako, na
rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.
Namshukuru
Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile
nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana. Nami natamani
sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha; nikiikumbuka Imani
uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na
katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.
Kwa
sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yao kwa
kuwekewa mikono yangu. Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya
upendo na ya moyo wa kiasi. Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala
usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya
Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
16:1-2, 5, 7-8, 11 (K) 5
(K)
Bwana ndiye fungu la posho langu.
Mungu,
unihifadhi mimi,
Kwa
maana nakukimbilia Wewe.
Nimemwambia
Bwana, Ndiwe Bwana wangu,
Sina
wema ila utokao kwako. (K)
Nitamhimidi
Bwana aliyenipa shauri,
Naam,
mtima wangu umenifundisha usiku.
Nimemweka
Bwana mbele yangu daima,
Kwa
kuwa yako kuumeni kwangu, sitaondoshwa. (K)
Utanijulisha
njia ya uzima,
Mbele
za uso wako iko furaha tele,
Na
katika mkono wako wa kuume
Mna
mema ya milele (K)
SHANGILIO
Mt.
28:19-20
Aleluya,
aleluya,
Enendeni,
mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, Bwana anasema. Mimi nipo pamoja nanyi
siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Aleluya.
INJILI
Lk.
10:1-9
Bwana
aliweka wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na
kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda
kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika
mavuno yake. Enendeni; angalieni, nawatuma kama wana-kondoo kati ya mbwa-mwitu.
Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. Na nyumba
yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na akiwamo mwana
wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu. Basi,
kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi
amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele
yenu; wapozeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment