“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano,
Januari 13, 2021,
Juma
la 1 la Mwaka wa Kanisa
Ebr.
2:14 – 18
Mk.
1:29-39
Ndugu
zangu katika Kristo karibuni kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo
neno la Bwana katika injili yetu tunakutana na Yesu akitenda miujiza mingi,
watu wakifurahia. Lakini anatambua kwamba ni wengi walio na uhitaji na hivyo
anakataa kumilikiwa na kundi moja tu na kwenda sehemu nyingine kuwahubiria
wengine habari njema. Anatambua kwamba wahitaji ni wengi na hivyo anaamua
kuwafuata.
Injili
hii iwe kwetu fundisho kubwa ndugu zangu. Wengi wetu tunatabia ya kujishikiza
kwa watu wachache tu na kufanya nao kazi. Mwisho wa siku ni wao tu huishia
kufaidi na kuwatelekeza wengine. Tupambane na kishawishi cha kutaka kumilikiwa
na watu fulani tu au watu wa eneo fulani tu. Wahitaji ni wengi. Tutoke tuende
mbali zaidi.
Somo
hili litusaidie pia sisi sote tulio na vyeo au madaraka au ujuzi mbalimbali.
Tushirikishane ujuzi huu na watu wa aina zote. Ofisi zetu ziwapokee watu wa
aina zote. Matajiri, maskini, makabila na dini zote. Kristo hakubagua.
Tusikubali kuvimbishwa vichwa na sifa chache za watu na kutekwa kirahisi.
Katika
somo la kwanza, tunaelezwa juu ya ubora wa Kristo kama kuhani mkuu. Yeye ni
kuhani bora anayeweza kuchukuliana nasi kwani alikubali kuchukua hali
yetu-anatambua mateso yetu na udhaifu wetu na hivyo aweza kutuombea vyema
machoni pa Baba. Hili tunaliona vyema katika injili ambapo anatambua maumivu ya
wanadamu na kuwaponya.
Nasi
ndugu zangu tusiogope kumlilia Yesu. Yeye ajua hali yetu yote, ajua ugumu
tunaopitia. Hakuna anayeielewa hali ya mwanadamu kama Yesu. Hivyo yeye ndiye wa
kuelezwa shida. Tuwapelekee pia wengine Yesu ili nao wapate kusikilizwa shida
zao. Kama mama mkwe wa Simon asingaliletewa Yesu, hakika asingalipona. Sisi
tuwapelekee wengine Yesu. Tusiwapeleke kwenye ushirikina. Tuwapelekee Yesu.
Hakika maisha yao yatakuwa bora zaidi.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment