MASOMO
YA MISA, JANUARI 13, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 1 LA MWAKA
SOMO
1
Ebr.
2:14 – 18
Kwa
kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo
hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani,
Ibilisi, awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti
walikuwa katika hali ya utumwa.; maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila
atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake
katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo
ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Na kwa kuwa mwenyewe
aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
105:1 – 4, 6 – 9 (K) 8
(K)
Bwana analikumbuka agano lake milele.
Mshukuruni
Bwana, liitieni jina lake,
Wajulisheni
watu matendo yake.
Mwimbieni
kwa zaburi,
Zitafakarini
ajabu zake zote. (K)
Jisifuni
kwa jina lake takatifu,
Na
ufurahi moyo wao wamtafutao Bwana,
Mtakeni
Bwana na nguvu zake,
Utafuteni
uso wake siku zote. (K)
Enyi
wana wa Ibrahimu, mtumishi wake;
Enyi
wana wa Yakobo wateule wake.
Yeye
Bwana, ndiye Mungu wetu;
Duniani
mwote mna hukumu zake. (K)
Analikumbuka
agano lake milele,
Neno
lile aliloviamuru vizazi elfu.
Agano
alilofanya na Ibrahimu,
Na
uapo wake kwa Isaka. (K)
SHANGILIO
Efe.
1:17, 18
Aleluya,
aleluya,
Mungu
wa Bwana wetu Yesu Kristo, awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.
INJILI
Mk.
1:29-39
Siku
ile, Yesu alipotoka katika sinagogi, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea,
pamoja na Yakobo na Yohane. Naye mkewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani,
hawezi homa; na mara wakamwambia habari zake. Akamkaribia, akamwinua kwa
kumshika mkono, homa ikamwacha, akawatumikia.
Hata
kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa
hawawezi, na wenye pepo. Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni. Akaponya
wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo
kunena, kwa sababu walimjua.
Hata
alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na
watu, akaomba huko. Simoni na wenziwe wakamfuata; nao walipomwona wakamwambia,
Watu wote wanakutafuta. Akawaambia, Twendeni mahali pengine, mpaka vijiji
vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana kwa hiyo nalitokea. Akaenda
akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment