“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatano
Januari 27, 2021.
JUMA
LA 3 LA MWAKA
Ebr.10:11
– 18
Mk.
4:1-20
Ukuhani
wa Melkisedeki ni mkuu kuliko wa taifa la Israeli
Karibuni
sana ndugu zangu wapendwa kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Leo
neno la Bwana katika somo la kwanza linatueleza juu ya ukuu wa ukuhani wa
Kristo. Zaburi yetu ya wimbo wa katikati inatuambia kwamba yeye ni kuhani
milele kufuatana na ukuhani wa Melkisedeki. Ukuhani wa Melkisedeki ni mkuu
kuliko wa taifa la Israeli, Baba wa taifa la Israeli yaani Abraham alikwenda
kwa Melkisedeki na kunyenyekea na kuomba Baraka.
Hivyo
hakuna mzao wa Abrahamu aliyekuwa na ukuhani ulioweza kumfikia Melkisedeki,
wazao wote wa Abrahamu wanapaswa kwenda kwa Melkisedeki na kubarikiwa. Ukuhani
wa Yesu ni wa Kimelkisedeki: ni wa Milele na ni mkuu kuliko wa wana wote wa
Abrahamu, hivyo wana wote wa Abrahamu ni lazima waende kwake kupewa baraka. Na
pia sadaka aitoayo yeye huondoa dhambi zote, damu yake ina thamani kubwa kwani
ni damu ya Mungu inayomwagika na hivyo huondoa dhambi kwa ubora kabisa.
Yote
haya yaonesha ukuu na ubora wa Kristo. Kristo ameshakuja, ya zamani tuyaache.
Ukuu wa damu yake utuongezee imani na kumpokea na kumwabudu zaidi. Tujifunike
na damu ya Yesu, afunike kazi zetu, na kwa namna ya pekee afunike na afya zetu.
Afya
zetu zipo hatarini kutokana na ueneaji wa sumu katika udongo, hewa, mimea, na
vyakula. Vyote hivi vinaiweka afya zetu hatarini, pia teknologia inavyoongezeka
imesababisha wakati mwingine afya zetu kuzorota. Magonjwa yanaongezeka kila
siku, tuzifunike afya zetu kwa damu ya Yesu.
Katika
injili, Yesu anatumia mfano wa mpanzi kuelezea mioyo mbalimbali inayopokea neno
lake. Mioyo hubarikiwa kwa kadiri ilivyojifunua kuupokea ujumbe wa Mungu. Mioyo
iliyojifunga ilishindwa kufaidi utajiri wa neno la Mungu. Tuache kuwa wachoyo
kwa neno la Mungu-uchoyo kwa Mungu unatukosesha mengi. Ulimkosesha Solomoni
ufalme katika nyumba yake, baada ya kufa kwake, familia ya Daudi ilipoteza
makabila kumi.
Wengi
wetu tuna hali mbaya kwa sababu ya uchoyo kwa Mungu. Tunajitetea mno kwamba
sisi ni maskini, hatuna cha kumpa Mungu-na kumbe ni uchoyo tu. Sisi tuache
uchoyo na hakika Bwana atatubariki zaidi. Tumsifu Yesu Kristo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment