MASOMO
YA MISA, JANUARI 27, 2021
JUMATANO,
JUMA LA 3 LA MWAKA
SOMO
1
Ebr.10:11
– 18
Kila
kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara
nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi. Lakini huyu, alipokwisha kutoa
kwa ajili ya dhambi dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa
Mungu; tangu hapo akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake.
Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa. Na roho
Mtakatifu naye atushuhudia; kwa maana, baada ya kusema, Hili ni agano nitakaloagana
nao baada ya siku zile, anena Bwana. Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, na
katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo, dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka
tena kabisa. Basi ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya
dhambi.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
110:1 – 4 (K) 4
(K)
Wewe ndiwe kuhani hata milele, kwa mfano wa Melkisedeki.
Neno
la Bwana kwa Bwana wangu,
Uketi
mkono wangu wa kuume,
Hata
niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako. (K)
Bwana
atainyosha toka Sayuni fimbo ya nguvu zako.
Uwe
na enzi kati ya adui zako. (K)
Watu
wako wanajitoa kwa hiari, siku ya uwezo wako,
Kwa
uzuri wa utakatifu
Tokea
tumbo la asubuhi,
Unao
umande wa ujana wako. (K)
Bwana
ameapa, wala hataghairi,
Ndiwe
kuhani hata milele
Kwa
mfano wa Melkisedeki. (K)
SHANGILIO
Yak.
1:21
Aleluya,
aleluya,
Pokeeni
kwa upole Neno la Mungu lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.
Aleluya.
INJILI
Mk.
4:1-20
Yesu
alianza kufundisha tena kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkubwa mno,
hata yeye akapanda chomboni, akakaa baharini; mkutano wote ulikuwako juu ya
nchi kavu kando ya bahari. Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, akawaambia
katika mafundisho yake, Sikilizeni; Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda; ikawa
alipokuwa akipanda, mbegu nyingine ilianguka kando ya njia, wakaja ndege
wakaila. Nyingine ikaanguka penye mwamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara
ikaota kwa kuwa na udongo haba; hata jua lilipozuka iliungua, na kwa kuwa haina
mizizi ikanyauka. Nyingine ikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikaisonga,
isizae matunda. Nyingine zikaanguka penye udongo ulio mzuri, zikazaa matunda,
zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia. Akasema,
Aliye na masikio ya kusikia, na asikie.
Naye
alipokuwa peke yake, wale watu waliomzunguka, na wale Thenashara, walimwuliza
habari za ile mifano. Akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa
Mungu, bali kwa wale walio nje yote hufanywa kwa mifano, Ili wakitazama
watazame, wasione, na wakisikia wasikie, wasielewe; wasije wakaongoka, na
kusamehewa.
Akawaambia,
Hamjui mfano huu? Basi mifano yote mtaitambuaje? Mpanzi huyo hulipanda neno.
Hawa ndio walio kando ya njia, lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara
huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao. Kadhalika na hawa
ndio wapandwao penye miamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, mara
hulipokea kwa furaha; ila hawana mizizi ndani yao, bali hudumu muda mchache;
kisha ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara hujikwaa. Na hawa
ndio wale wapandwao penye miiba, ni watu walisikiao lile neno, na shughuli za
dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga
lile neno, likawa halizai. Na hawa ndio waliopandwa penye udongo ulio mzuri; ni
watu walisikialo lile neno na kulipokea, na kuzaa matunda, mmoja thelathini,
mmoja sitini, na mmoja mia.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment