“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi,
Januari 2, 2021,
Juma
kabla ya Epifania
Kumbukumbu
ya Watakatifu Basili Mkuu na Gregori Nazienzi
1
Yoh 2:22-28;
Zab
98: 1-4;
Yn
1:19-28.
UBATIZO,
UHAI MPYA WA NEEMA.
Karibuni
ndugu zangu katika adhimisho la misa Takatifu. Leo tunafanya kumbukumbu ya
Watakatifu Basili na Greogori Nazianzeni, Maaskofu na Walimu wa Kanisa.
Tunachojifunza
kikubwa katika Masomo yetu ni Ukuu alionao Kristo: Yesu aliyezaliwa duniani ni
nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu. Yohane katika somo la kwanza anasema kwamba
yeye (Yesu) ameunganika na Baba kwa undani wa pekee kiasi kwamba kila amkanaye
Yesu, humkana na Baba pia. Huyo hatakuwa na mtetezi kwani Yesu ndiye hakimu na
Baba amempa mamlaka juu ya vyote.
Yohane
Mbatizaji katika injili ya leo haoni aibu kuushuhudia ukuu wa Yesu kwamba ni
mkuu kuliko yeye kiasi kwamba hastahili hata kulegeza gidamu ya viatu vyake.
Watakatifu Bazili Mkuu na Gregory Nazianze wanasifika kwa umahiri wao katika
kuutetea Umungu wa huyu Yesu. Kwa pamoja waliupinga uzushi wa Ariani uliokataa
ukuu na umoja wa Umungu wa Baba na wa Mwana. Watakatifu hawa wanaunganika na
Yohane katika somo la kwanza kutuambia kwamba tukae ndani ya Kristo na
tuyakatae mafundisho yote yanayompinga Kristo. Kazi tunazofanya zimtangaze
Kristo; Tumshuhudie nyakati zote na mahali pote
Tumuombe
Yesu tukisema, Ee Yesu uliyezaliwa duniani, nisaidie nisione aibu kukushuhudia
wewe kwa maneno yangu, mawazo na matendo yangu.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment