MASOMO
YA MISA JANUARI 2, 2021
JUMAMOSI
KUMBUKUMBU
YA WATAKATIFU BASILI MKUU NA GREGORI WA NAZIENZI
SOMO
1
1Yn
2:22-28
Wapenzi:
ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga
Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana. Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye
Mwana anaye Baba pia. Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani
yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi
mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba. Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia,
yaani, uzima wa milele.
Nimewaandikia
haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. Nanyi, mafuta yale mliyoyapata
kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama
mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si
uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake. Na sasa, watoto wadogo,
kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibike
mbele zake katika kuja kwake.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
98:1-4 (K) 36
(K)
Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Mwimbieni
Bwana wimbo mpya,
Kwa
maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono
wa kuume wake mwenyewe,
Mkono
wake mtakatifu umemtendea wokovu. (K)
Bwana
ameufunua wokovu wake,
Machoni
pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
Amezikumbuka
rehema zake,
Na
uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. (K)
Miisho
yote ya dunia imeuona,
Wokovu
wa Mungu wetu.
Mshangilieni
Bwana, nchi yote,
Inueni
sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Siku
takatifu imetung’aria: Enyi mataifa njoni mkambwabudu Bwana: Kwa sababu mwanga
mkubwa umeshuka duniani.
Aleluya.
INJILI
Yn.
1:19-28
Na
huu ndio ushuhuda wake Yohane, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi
kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? Naye alikiri, wala hakukana;
alikiri kwamba, Mimi siye Kristu. Wakamwuliza, Ni nani basi? U Eliya wewe?
Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu La. Basi wakamwambia, U nani?
Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? Akasema, Mimi ni
sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena
nabii Isaya. Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo. Wakamwuliza,
wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii
yule? Yohane akawajibu akisema, Mimi nabatiza na maji. Katikati yenu amesimama
yeye msiyemjua ninyi. Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili
kuilegeza gidamu ya kiatu chake. Hayo yalifanyika huko Bethania ng’ambo ya
Yordani, alikokuwako Yohane akibatiza.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment