“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi
Januari 28, 2021.
JUMA
LA 3 LA MWAKA
Ebr
10: 19-25;
Zab
24: 1-6;
Mk
4: 21-25
------------------------------------------------
MWANGA
WENU UANGAZE
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Zaburi yetu ya wimbo
wa katikati leo inatueleza habari za yule atakayepanda mlima mtakatifu wa
Mungu. Huyu ni yule aliye na mikono safi na moyo mweupe, asiyeamini miungu ya
uongo au kumsengenya jirani yake.
Ndugu
zangu, kiukweli, ulimwenguni kuweza kukutana na mtu kama huyu ni vigumu sana
kwani ulimwenguni huishi wanadamu na si malaika. Lakini somo la kwanza
linatupatia matumaini makubwa juu ya hili-kwamba Yesu ndiye mwenye kutuwezesha
kuupanda huu mlima mtakatifu. Yesu ni kuhani mkuu, yeye ndiye mwenye kutupatanisha
na Baba, tunaweza kupaingia patakatifu kwa DAMU YA YESU.
Yesu
ndiye mwenye kutupatia ujaasiri wa kupaingia patakatifu. Hivyo tuthamini ukuu
wa damu hii, ndiyo inayotuokoa.Tukifunikwa na damu hii, hakika hakuna
kitakachotusumbua, tunapata ujasiri wa kupaingia patakatifu. Leo tuombe
kufunikwa na damu hii. Usipite bila kumwambia Mungu hili kwamba nifunike kwa
damu yako nipate kupaingia patakatifu. Sentensi moja tu yaweza kuokoa maisha
yako na maoteo yote ya yule mwovu.
Katika
injili, Yesu anatumia mfano kwamba taa lazima iwekwe juu ya kiwango ili ipate
kuwaangazia wengine. Sisi kwa ubatizo wetu ni taa ya ulimwengu-na huwa
tunajitahidi kujiweka juu ya kiwango ili tutoe mwanga. Lakini shida ni kwamba
hatutoi mwanga wowote na ndio maana hatujulikani kwamba tupo. Hii ni kwa sababu
taa isiyotoa mwanga sio rahisi kuonekana. Inahitaji itoe mwanga ili yenyewe
ipate kuonekana na kuwaangazia wengine.
Sisi
tutambue kwamba tunangaa kutokana na matendo mema na Sala. Hapa ndio tunapata
kutoa mwanga. Bila haya, maisha yetu kama wakristo huwa na kasoro. Tusiache
kusali na kufanya matendo mema. Injili yetu inatuambia kwamba tukifanya haya
tutapokea kuendana na kipimo tulichotoa, naye Bwana atatubariki hivyo hivyo.
Tumsifu Yesu Kristo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment