MASOMO
YA MISA, JANUARI 28, 2021
ALHAMISI,
JUMA LA 3 LA MWAKA
SOMO
1
Ebr.
10:19 – 25
Ndugu,
kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile
aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake; na
kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; na tukaribie wenye moyo wa kweli,
kwa utimilifu wa Imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya;
tumeoshwa miili kwa maji safi. Na tulishike sana ungamo la tumaini letu,
lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu; tukaangaliane sisi kwa sisi na
kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; wala tusiache kukusanyika pamoja, kama
ilivyo desturi iya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri
mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
24:1 – 6 (K) 6
(K)
Hiki ndicho kizazi cha wautafutao uso wako, Ee Bwana.
Nchi
na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,
Dunia
na wote wakaao ndani yake.
Maana
ameiweka misingi yake juu ya bahari,
Na
juu ya miti ya maji aliithibitisha. (K)
Ni
nani atakayepanda katika mlima wa Bwana?
Ni
nani atakayesimama katika patakatifu pake?
Mtu
aliye na moyo safi na moyo mweupe
Asiyeiinua
nafsi yake kwa ubatili,
Wala
hakuapa kwa hila. (K)
Atapokea
Baraka kwa Bwana,
Na
haki kwa Mungu wa wokovu wake.
Hiki
ndicho kizazi cha wamtafutao,
Wakutafutao
uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. (K)
SHANGILIO
1Pet.
1:25
Aleluya,
aleluya,
Neno
la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa
kwenu.
Aleluya.
INJILI
Mk.
4:21-25
Yesu
aliwaambia wafuasi wake: Mwaonaje? Taa huja ili kuwekwa chini ya pishi, au
mvunguni? Si kuwekwa juu ya kiango? Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila
makusudi lije likadhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila makusudi lije
likatokea wazi. Mtu akiwa na masikio ya kusikia, na asikie.
Akawaambia,
Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena
mtazidishiwa. Kwa maana mwenye kitu atapewa, naye asiye na kitu, hata kile
alicho nacho atanyang’anywa.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment